#MAJIRA YAKO HATMA YAKO [TAMBUA MAJIRA YA BWANA?]

High season(nyakati ya utele) kwa kila mwanadamu chini ya jua ni haki ya msingi na ya upendeleo kutoka kwa Bwana ila sharti uitambue ili iwe ya manufaa kwako na kizazi chako.  Kuna majira ya kila jambo chini ya jua, na majira  ya mwanadamu hayalazimishwi wala kuzuiliwa na yeyote, katika Luka 9:44-45 tunaona Yesu Kristo akiwaambia wanafunzi ya kuwa, “ Yashikeni maneno haya masikioni mwenu,........ Lakini biblia inasema "hawakufahamu neno lile, likafichwa kwao wasilitambue...”. Ona sasa pasipo majira kutimia hakuna namna mwanadamu anawezapata ufahamu wa jambo, suluhisho ama taarifa inayomuhusu na kuielewa ama kuiamini kabisa mpaka majira rasmi ndipo huwa nguvu kwake.
Luka 19:42-44, Yesu Kristo anasisitiza na kuhuzunishwa kuhusu wanadamu na utambuzi wa majira rasmi. Mhubiri 3:1-8, Mfalme Sulemani anasisitiza ya kwamba ziko nyakati tofauti mwanadamu anapaswa kufahamu ili aishi vyema na kimafanikio kabisa.
Isaya 61:1-2, Yesu Kristo mwenyewe anatoa tamko kwamba amekuja kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa, sasa hayo ni majira na tunaona vyema kabisa baada ya tamko hilo alilolinena hekaluni mbele ya viongozi wa dini wote, mambo ambayo alikuja kuyatenda baadaye yakaja kuwa gumzo katika nchi yote. Lakini ukifuatilia kabla ya tamko hili utaona alikuwa akiombwa kufanya jambo kwa uweza ndani yake alikataa na kusema saa yangu bado. Hivyo basi hakuna mwanadamu anayeweza kufaulu, kuvuka, kushinda, kufanikiwa pasipo kujua majira ya Bwana katika maisha yake.

Na ndio maana mhubiri 9:11 anasistiza kuwa wakati na bahati huwapata wote, sio uwezo wako bali wakati uliopangiwa au kuamuriwa na Bwana ndio dira ya mafanikio ili kuifikia ile hatma yako.
Siri ya majira ni kwamba pale unapoyatambua majira ni mwanzo mpya wenye hatma yako.
Kutambua majira hutengeneza utayari ndani ya mwanadamu.
Kutambua majira huimarisha imani ya mwanadamu.
Kutambua majira humfanyia mwanadamu focus ya maisha sahihi.
Kutambua majira ni mwanzo wa hitimisho la jambo lililokusudiwa na Bwana.
Hata Malaika mwenyewe hawezi zuia majira yako isipokuwa mwanadamu mwenyewe.

A] FAIDA ZA KUTAMBUA MAJIRA KWA MIFANO YA BIBLIA
Mfano wa watu wa Mungu katika Biblia ambao walitambua majira ya Bwana wakabarikiwa na kuneemeshwa na Bwana;
Ibrahimu, Mordekai/Esta (Esta 4:13-14), Mama Mshunani ( 2 Wafalme 4:2, 8-36 (10)), Koreshi (Ezra 1:!-12, 2 Nyakati 36:22-23), Mama wa Sarepta – Mjane (1 Wafalme 17:9-24), Daniel 9:2-27, Wenye ukoma wane (2 wafalme 7:3), Nehemia 1:1-5, Nuhu (Mwanzo 6), Henoko (Mwanzo 5:21-24), Musa (Kutoka 2:11-15), Hanna (1 Samweli 1:9-20), Elisha (1 Wafalme 19:19-21 na 2 Wafalme 2), Mamajusi (Mathayo 2:1-2), Wachunga kondoo (Luka 2:8-18), Simeoni na Anna Fanueli nabii mke (Luka 2:25-38).

B] ATHARI ZA KUTOTAMBUA MAJIRA KWA MIFANO YA BIBLIA
Baadhi ya mifano ya watu wa Mungu ambao kwenye biblia walipata hasara, walikosa walivyopasa kupata, walijuta ama kuathirika vibaya baada ya kutokutambua majira rasmi ya Bwana;
Kaini, Esau, Mfalme Sauli, Akida (2 Wafalme 7:3), Zakaria (Luka 1:11-23), Samsoni (Waamuzi 14), Petro, Paulo, kaka zake Yusufu na kaka zake Daudi.

Pasipo kutambua majira sahihi kuna uharibifu wa nafsi ya mwanadamu, na ucheleweshwaji wa Baraka pia. Kuna usemi usemao “Ignorance of law has no excuse, no defence”, yule asiyeyatambua majira yake hana pato bali kukabiliana na hasara na matokeo yatokanayo na upuuzi huo, hivyo basi nami nasema kutokujua majira sio ngao ni kwamba utakosa ulichopaswa kupata na kuishi maisha yasiyokusudiwa na Bwana i.e. utatembea jangwaani na gizani kwa kule kutokujua majira.
Wanadamu mara zingine hawatambua majira yao rasmi kwa sababu ya kupuuza nyakati, kufungwa na nguvu za giza, laana zitokanazo na maagano ya mizimu, matambiko ya ukoo, nira za kichawi na kiganga, ibada za sanamu na miungu, kughairi pindi wapatapo misukosuko, kutochukua hatua sahihi, kukosa washauri na baba wa kiroho ama kutowashirikisha wenye uelewa, kutokuwa na kawaida ya kusali mara kwa mara yaani kujiweka karibu na Mungu huku ukidumisha uhusiano imara na roho mtakatifu, au kule kutotambua saa ya kutembelewa na wenyeji wa mbinguni (heavenly visitations).
Lakini ukweli ni kwamba kama wanyama ama mimea ama miti hutambua majira rasmi na kujiongeza sawasawa na vile ilivyokusudiwa na Bwana, Je? Si zaidi wanadamu wenye utashi kamili kuzidi wao. Na hii ni kweli kabisa hata nyumbu hutambua majira rasmi na kuchukua hatua stahiki kulinda uhai wao.

Mpendwa katika Bwana, kama vile Yesu Kristo alivyosema katika Luka 19:42-44, ya kwamba laiti ungalijua siku na saa ikupasayo amani wewe msomaji wangu ungalichukua hatua muhimu sasa kumuelekea yeye atoaye uzima bure, amani bure, afya bure na tiketi ya kuingia mbinguni bure kabisa. Chukua hatua sasa ambayo ni muhimu sana kwa maisha yako kwa kumfanya Yesu Kristo Bwana na mwokozi wa maisha yako hakika yaliyofichwa yatafumbuliwa kwako, na hatua yako yaani huo utayari wako na uamuzi wako ni dhahiri kwamba hatma yako ni njema kabisa na nuru ya Bwana imeangaza kwako sasa (Isaya 60:1) Arise Shine!!, Hallelujah!!, Amina.

2 comments: