Thursday, August 29, 2019

#MY CONFESSION ABOUT 'MY STRENGTH & MY SAVIOUR JESUS CHRIST OF NAZARETH'

It is those challenging circumstances in life, daily struggles and troubles, among other factors that lead human being to know who really God is, and at last man declares authority and power of Him, God who is robed in majesty and who alone worthy of all the glory. And indeed Bible clearly declares in Daniel 11:32 that; " ......, the people who know their God shall be strong and carry out great exploits."

According to the might acts that God did in that time through signs, miracles and wonders to the mighty men recorded in the holy bible, they were never ashamed of glorifying Him majestically.
In the book of Exodus 15:2, Moses said; "The LORD is my strength". 
In the book  of Psalm 118:14, King David said; "The LORD is my strength". 
And in the book of Isaiah 12:2, Isaiah the Prophet said; "The LORD JEHOVAH is my strength". Hakika BWANA ni nguvu zangu, even I (Gpc), declares that; "Jesus Christ is my Power - Yesu Kristo ni nguvu zangu", Ni wimbo wangu, Nami nitamsifu daima naye amekuwa Wokovu wangu na Mungu wangu nitamtukuza milele yote.

Na huu ndio ukiri wangu (my confession) for life as a Gpc:
I AM GOD'S POWER CONTAINER (Gpc), THAT POWER CONTAINED IN ME IS ACTUALLY OF GOD, JESUS CHRIST OF NAZARETH IS THAT POWER.
                      
                       "I AM GOD'S POWER CONTAINER,
                        JESUS CHRIST IS MY POWER."

Therefore, brethren contain the God's power in Christ Jesus of Nazareth.

Stay blessed, Amen.

Monday, August 5, 2019

#NDUGU WA KWELI (YESU wa Nazareti)


Ndugu wa kweli ni kimaanisha ndugu wa damu, kila mwanadamu ana ndugu wa damu ambao kwa hao ameunganishwa nao iwe kwa kuzaliwa pamoja, ama wazawa wa walio ndugu upande wa baba na wa mama hii hudhihirishwa kwa kushabihiana kwa baadhi ya tabia zao, sura zao, kimuonekano na mifanano mingine mingi ya ndani na nje ya mwili inayoonyesha muunganiko wao kama ndugu. Sasa kwenye sayansi kuna kitu huzungumziwa sana kinachoitwa “DNA” ambacho ndicho kipimo kitumiwacho kutambua "vinasaba" kati ya mwana-damu mmoja na mwingine kama kweli ni ndugu yako awe mwanao, kaka, dada, binamu, baba, mama, shangazi, mjomba na ndugu wote wa damu. Na ukisoma Torati ya Musa kwa umakini katika Biblia kitabu cha mambo ya walawi 25: 47-52 (soma sura ya 25 yote) inasema hakika haiwezekani kabisa mtu asiye ndugu yako kukukomboa na sisi tunakiri ya kuwa Yesu Kristo wa Nazareti alitukomboa sisi kwa damu yake na kwa mauti ya msalaba.
Je, kwa hivyo twaweza sema Yesu wa Nazareti ni ndugu yetu? Kwa maana ndiye aliyetukomboa utumwani wa dhambi, na je ni ndugu yetu kweli?.
Hapo utaona inachanganya sana lakini nikusihi hivi, ukitafakari kwa kina Neno la Mungu na kwa sala ndipo utajua Yesu Kristo wa Nazareti ni ndugu yetu hakika, kwa kuwa biblia imethibitisha hivyo;
v  katika kitabu cha waefeso 4:6 kuwa Yesu wa Nazareti ni Baba yetu, Baba wa wote. 
v  Na katika wagalatia 4:19 biblia takatifu inasema Yesu wa Nazareti ni mama yetu aliyetuazaa (tulizaliwa mara ya pili katika Yeye).
v  Katika kitabu cha mithali 7:3-4 biblia takatifu inasema Yesu wa Nazareti ni dada yetu
v  Katika kitabu cha Waebrania 2:11 biblia takatifu inasema Yesu wa Nazareti ni kaka yetu
v  Katika kitabu cha Mambo ya Walawi 25:49 biblia takatifu inasema Yesu wa Nazareti ni binamu yetu na mjomba wetu
Kwa hiyo sasa twatambua hakika yakuwa yeye Yesu wa Nazareti ni vyote katika vyote, kwa namna ambayo biblia takatifu katika waefeso sura ya 4:8-10 inasema kitu kimoja cha kushangaza ya kwamba yeye Yesu wa Nazareti alienda juu sana kupita mbingu zote, kwa hiyo yuko juu ya vyote, na pia biblia takatifu (1 Timotheo 2:5) inasema yeye ni mpatanishi na mwakilishi wetu kwa hivyo yuko katikati yetu, na tena inasema (1 Wakorintho 3:11)yeye ni msingi wetu kwa hivyo yuko chini pia. Siyo hivyo tu bali biblia kwenye kitabu cha ufunuo 1:8; 1:17 inasema kitu kimoja cha ajabu sana kuwa yeye Yesu wa Nazareti (Kristo) ni Alfa na Omega, ndiye mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho kwa hivyo yuko katika miisho yote. Na biblia takatifu inamalizia katika 1 Wakorintho 6:17 kwa kusema yeye yule aliyeungwa na Bwana Yesu Kristo wa Nazareti ina maana baada ya wokovu ni roho moja naye ikimaanisha, ule wokovu wake mkuu kama ndugu yetu unakufanya kuwa zaidi ya ndugu yaani ni roho moja naye na hapo huwezi kutofautishwa naye.
Hivyo niwaambia ndugu zangu huyu Yesu Kristo wa Nazareti ninayemtaja hapa hakika ni mkombozi wa dunia kwa kuwa anakidhi na kutimiza yote yamfanyao ndugu yetu na mkombozi wetu, tambua leo, kata shauri dakika hii, amini na amua sasa naye atakuweka huru huru kweli nawe utaishi katika neema yake maisha yako yote hutasaritiwa naye kamwe kwa kuwa ni baba, ni mama, ni dada, ni kaka, ni binamu na mjomba, ni wa juu sana, uu kati yetu na chini pia na pale tu ukiamua kuokoka wawa roho moja naye yaani zaidi ya ndugu wala huwezi kutofautishwa naye.
Okoka leo kwa uweza wa roho mtakatifu naye atakukomboa hakika na atakutenga na dhambi zote ulizokuwa umefungwa nazo maishani mwako, amina.