Monday, July 14, 2025

#ARE YOU; A MARTHA OR A MARY?


Je, wewe ni Martha au Mariam?,  Jiulize.......

Luka 10:38-42

Mara YESU alipokuwa karibu MARTHA alikuwa wa kwanza kumlaki na kumkaribisha.

YESU alipokuwa kati yao:

ni MARIAM ndiye aliyeketi miguuni mwake Yesu kujifunza na kusikiliza maneno ya YESU.

MARTHA alikuwa akihangaika kwa utumishi mwingi, kusumbuka na kufadhaika kwa ajili ya vitu vingi uweponi wa Bwana huku akimwacha YESU na umbu lake (kama kumuandalia chakula jibu la YESU ni Yohana 4:31-34).

YESU aliweka wazi na kufunguka msingi wa yote unaotakiwa na wote; ambao ni mmoja tu kukaa karibu naye YESU, kumkaribia yeye huku moyo umemufungulia. Fungu hilo jema ndiyo wakina MARIAM huchagua lidumu kwao.


Hata wakati wa Kifo cha Lazaro kaka yao:

Yohana 11:20-27

YESU alipofika uweponi mwao karibu nao, MARTHA pekee yake kutoka msibani alikuwa wa kwanza kumlaki.

Neno alilolisema MARTHA kwa YESU "KAMA UNGALIKUWAPO HAPA NDUGU YANGU HANGALIKUFA". Kauli ile namna alivyoisema na imani yake ya kusitasita haikuleta matokeo mazuri bali iliprovoke/ilileta mjadala badala ya kuleta suluhisho kutoka kwa Bwana.

Yohana 11:28-44

Ni MARTHA pamoja na imani yake ya kuyumbayumba ndiye aliyeenda kumuita MARIAM umbu lake faraghani kufaidi uwepo wa Bwana akisema YESU yupo anakuita. Mahali palepale alipokutana na MARTHA ndipo YESU alikuwepo wala hakuondoka; anga lilelile, uwepo uleule, spoti ileile, mazingira yaleyale MARIAM akamwendea upesi. Lakini kwa moyo wa MARIAM ulivyokuwa alivyotoka msibani kwenda uweponi mwa Bwana si pekee bali wote waliokuwa naye walimfuata. MARIAM alipofika kwa Bwana, na kumwona YESU; ALIANGUKA MIGUUNI PAKE (Unyenyekevu wake ule ulikuwa mkuu sana na moyo uliofunguka wenye tumaini la kufungua mbingu na kumuona Mungu huku na imani thabiti kwa Bwana YESU isiyoyumbishwa na chochote), kwa huzuni na moyo ule wa imani uliofunguka kwa Bwana huku akiwa na matarajio ya matokeo mema. MARIAM akainena kauli ileile kama ya MARTHA kwa namna yake kuwa "KAMA UNGALIKUWAPO HAPA NDUGU YANGU HANGALIKUFA".  YESU alipoona huzuni yake juu ya jambo lile na kulia kwake kwa uchungu kama mwenye mzigo mkuu ktk msiba ule kwa namna alivyoinena kauli ile kuliko hata MARTHA alivyojipresent/ alivyojihudhurisha kwake Bwana, kwa maana kwa kulia kwake MARIAM kwa uchungu kuliprovoke/kuliibua kilio kikuu hata kwa wale waliokuwa wamefuatana naye. Ndipo YESU ALIUGUA ROHONI, AKAFADHAIKA ROHO YAKE. 

YESU ALILIA MACHOZI HUKU AKIUGUA NAFSINI  MWAKE, alipoona tu kaburi alimowekwa Lazaro, AKALIA KWA SAUTI KUU mpaka Lazaro akafufuka. 

Hii yote ilitokea sababu ya namna MARIAM alivyonyenyekea na kumheshimu YESU kwa hisia ya kweli na ya dhati moyoni mwake mbele za wote msibani kuliko MARTHA (japo naye MARTHA anasehemu yake ktk utimilifu wa jambo lile, kuachwa kwake na uwepo ule wa Mungu ktk Bwana YESU ni changamoto kuu ambayo ufalme wa mbinguni unakutana nayo hata sasa kwa wengi, wengi wapo eneo sahihi, wakati sahihi na wengine wanatumika humo ila wanakosea namna ya kuaccess vya rohoni kutoka kwake YESU kwa kutokuelewa vema namna yake ya kumpokea Roho wake Mtakatifu).

Kinamna ile MARIAM alivuta uwepo wa Mungu, aliprovoke presence ya Mungu na mbingu yake ktk Bwana Yesu kuleta matokeo yaliyoonyesha utukufu wa Mungu katika jamii yao yote. Sasa pamoja na hayo yote kutukia machoni pake MARTHA bado tunaona jinsi alivyokuwa mkavu uweponi mwa Bwana YESU pasipo kuwa na imani thabiti na moyo uliofunguka; hata akaja kumwambia YESU pamoja na ufahamu aliomupa mwanzoni akasema; marehemu ananuka sasa amekuwa maiti, kwa hatua ile Bwana YESU alimkemea kama kusema na shetani mpinzani wake (ndani ya MARTHA kwa kuwa ndiye aliyefungua mlango wa kusitasita ktk imani yake).

Jamii ya MARTHA kama wadhifu wake ktk biblia ni kama Mpigadebe fulani hivi kuwaambia mwenzake ingia usafiri na gari kwa ushawishi mkubwa lakini yeye hubaki hapo hapo huku akiacha kina MARIAM wakiexperience the goodness of the journey. Ndivyo ilivyo hata katika Bwana usiwe wa jamii ya MARTHA bali kuwa kama MARIAM.

Ndipo utajua mwenyewe unao ufungua wa kuufungulia ukuu wa Mungu ndani yako utakaofurika maishani mwako na YESU yeye yupo siku zote karibu na moyo wako abisha ili ajifunue ndani yako kwa namna ya ajabu. 

Kwa hivyo ni wewe kutune ile frequency ya moyo wako vizuri kwa ile mode/mood aitakayo, namna unavyojisikia ile hali yako ya ndani ya uhitaji, ile shauku kuu ya moyo wako huku ukimuelekea yeye, ukijimimina kwake, na utakapofika hali hiyo atajisikia pia ndani yake na hakutakuwa na pingamizi kwake tena kwa namna yoyote zaidi ya kujifunua kwako yaani Mungu na mbingu yake ndani yako ktk Bwana Yesu kristo unayempokea moyoni mwako kikamilifu kupitia Roho wake ayafunue yote mema maishani mwako. 

Be MIRIAMS AND NOT MARTHAS, brother and sister; enjoy God things easily🙏🏿.