#AKATEKA MATEKA, AKAWAPA WANADAMU VIPAWA [YESU WA NAZARETI]

Aliposema; “IMEKWISHA”, Ilikuwa ndio mwanzo wa kufunguka kwa majaliwa yako katika maeneo yote ya maisha yako ili kupokea miliki zako zote zilizokuwa zimeshikwa na mwizi shetani, sio tu afya wala utajiri pekee bali pamoja na vipawa vya roho mtakatifu vilihuishwa saa na wakati ule na roho wa BWANA; ufahamu, hekima, shauri, maarifa, uweza, hofu ya Mungu na kumcha Mungu.
Hii ina maanisha kwa uweza wa Roho mtakatifu tunavyo vyote ni jukumu letu kuvifanya halisi kwetu katika ulimwengu wa mwili.
Ikumbuke siku zote ile siku ya wokovu wako alioufanya Yesu Kristo ndani yako; na maanisha ile siku ya uhuru wako katika roho ili uwe huru katika yeye milele.
Huyo ni Yesu Kristo wa Nazareti; Akateka mateka, akawapa wanadamu vipawa.
Yesu ananipenda sana mimi; Nina hisia hiyo kwa nguvu sana moyoni mwangu, Ooh! YESU.
Ni vipi kuhusu wewe?
Mwalike leo moyoni mwako; Yesu atakubadilisha kwa wema na kuyabadilisha maisha yako hakika na kukupa umiliki wako wa awali ulioibiwa kwako.
Yatafakari maandiko haya ktk Biblia Takatifu; Yohana 19:30, Zaburi 68:18, Efeso 4:8-11, Isaya 11:2-3, Wakorintho wa Kwanza 12:8-10, Nahumu 2:9 na Waamuzi 5:12.

~Jina la Bwana wetu Yesu Kristo wa Nazareti libarikiwe na kuinuliwa juu sana milele yote, Amina.

No comments:

Post a Comment