#INUNUE KWELI

 “Inunue kweli, wala usiiuze;
Naam, hekima, na mafundisho, na ufahamu.”
Ndio! Usiiuze kweli, wanadamu wauliza maana yake nini neno hili?
Ndivyo ilivyo mpaka kweli itoweke moyoni mwako isiwepo tena ndipo utakapojua thamani na gharama yake, yaani kule kuikosa tena ile Kweli iliyokuwepo kwanza kwako, hii yaweza kuwa kwa kutokuiamini tena ama kuizoea kiasi ambacho inakuwa kama sio Nguvu za Mungu tena ndani yako.
Tafuta Ufalme wa Mungu kwanza,  gharamia katika hili; kwa moyo wako wote, kwa akili zako zote na kwa Nguvu zako zote, kwa maana imo thamani ndani ya Kweli, ambayo ni Uzima wa milele upatikanao katika YESU KRISTO, ambaye ndio Neno la Mungu na ni KWELI na MUNGU hakika.
[Mithali 23: 23]

"Buy the TRUTH and sell it not, also wisdom, and instruction, and understanding." 
[Proverbs 23:23]

No comments:

Post a Comment