#MPINGE SHETANI MKARIBIE MUNGU UISHI MAISHA YA USHINDI

   Biblia katika Yakobo 4:7-8 inatusisitiza tumpinge shetani na kujiweka chini ya Mungu kwa kumkaribie na mstari wa 10 inatuasa tunyenyekee mbele ya Bwana naye atatuinua, wala haijatupa msistizo kuwa tunyenyekea mbele ya wanadamu halafu ndio Bwana atuinue, no! hapana. Mwanadamu akizaliwa mara ya pili inamaana amekuwa kiumbe kipya lakini anaishi katika dunia ileile, ndio maana ukisoma sana biblia utaona kuna sehemu anasema yule mvumilivu akisha stahimili majaribu atapewa taji ya uzima ambayo Mungu amewaahidi wale wampendao (yakobo 1:12) na sehemu nyingine yule atakayevumilia mpaka mwisho ndiye atakayeokoka (Mathayo 24:13). Hapa tunaona ya kuwa kule kuendelea kuwepo duniani hata baada ya kuokoka kuna maanisha vita vingalipo, yaani kama mkristo unakuwa umenolewa sawasawa kimdhihirishia adui shetani kwa mapigo yake yote atakayoyaelekeza kwako ya kuwa wewe ni mshindi na mwana wa Mungu hakika katika kristo, yapo yeye shetani ni vigumu kukubali na hilo, lakini kwa kusimama kwako kutadhirisha kwamba ndio ukweli halisi.
Kwa hivyo tunaona ya kuwa kwa ule wokovu ulioupokea kutoka kwa Bwana dunia ndio itakupinga zaidi ya vile ilivyokunyanyasa kabla hujafanyika mwana wa Mungu. Hukumu ni mwisho yapo Shetani amekwishwa hukumiwa, nakuambiwa yeye na ufalme wake hawataacha kutafuta upenyo wa kukuangusha kama wewe wenyewe hutajiweka sawa na Yesu Kristo, ndio maana tunasisitizwa ya kuwa ukianguka tubu na ungama makosa yako yote kwa kuwa hakuna dhambi ndogo ili yule adui asiwe na haki ya kukudhuru tena na kukukwamishwa katika maisha yako.
Naam! utampingaje shetani? mpinge kama Yeremia 10:10-11 kwa kumdhihirishia na kuthibitishia kwamba BWANA ndio Mungu wako wa kweli,  Mungu aliye hai, Mfalme wa milele na ndiye aliyeumba mbingu na nchi na kwa ghadhabu yake hata nchi hutetemeka wala mataifa hawawezi stahimili hasira yake, na ya kuwa yeye shetani si kitu, na iambie miungu yote inayokufuatilia iwe mizimu, majini, mapepo ambayo hayaachi kukuzonga kisa yanajidai yanahati miliki ya ukoo na familia yako tangu vizazi vingi vilivyopita ambavyo hata wewe vingine huvifahamu. Sema leo ni mwisho na ya kwamba miungu haikufanya mbingu wala nchi hivyo iangamie katika nchi na kutoweka kabisa chini ya mbingu.
Amina, ishi maisha ya ushindi katika kristo.

No comments:

Post a Comment