#NGUVU INAYOSABABISHWA NA WATU WAISHIO KATIKA WASIFU (ASILI) WA YESU WA NAZARETI KUPITIA JINA LAKE

   Biblia takatifu katika waefeso 3:20 inasema; “Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu”, hivyo kuishi katika wasifu wa Yesu wa Nazareti kuna ujazo wa ajabu wa Nguvu za Mungu ndani yetu kwa njia ya roho mtakatifu.

Matendo 19:11-16; Mungu akafanya kwa mikono ya Paulo miujiza ya kupita kawaida, hata wagonjwa wakaletewa leso na nguo zilizotoka mwilini mwake magonjwa yao yakawaondokea,pepo wachafu wakawatoka. Baadhi ya wayahudi wenye kutanga-tanga, nao ni wapunga pepo, wakajaribu kutaja jina la Bwana Yesu juu yao waliopagawa na mapepo wachafu, wakisema Naapisha kwa Yesu, yule anayehubiriwa na Paulo. Walikuwapo wana saba wa mtu mmoja Skewa, myahudi, kuhani mkuu, walifanya hivyo. Yule pepo mchafu akawajibu akawaambia, Yesu namjua na Paulo namfahamu, lakini ninyi ni akina nani?.Na kisha yule mtu aliyepagawa na pepo akawarukia wawili, akawaweza na kuwashinda hata wakatoka mbio katika nyumba hali wa uchi na kujeruhiwa.

Ni rahisi kwa jiwe au punda kuzungumza na hata mlima kuhama kuliko mwanadamu aliyejaa maswali na udadisi kubadilishwa kwa uvuvio wa roho mtakatifu na kuwa na imani kama ya jiwe, punda, mifupa mikavu au mlima. Pointi yangu ni kwamba udadisi mwingi hufifisha na Kupunguza kabisa kiwango cha imani kwa namna ambayo hata hofu saa nyingine inaishinda imani. Kwa Yesu kristo wa Nazareti ni rahisi mtoto mdogo mwenye asilimia 0% ya kufikiri fikiri au punguwani au watu waaminio katika giza ama wapagani kupokea neema ya Mungu na kwenda mbinguni kuliko wana wa nuru ambao hudhani wenyewe kuwa wanahaki sana na kuishia jehanamu.

Mawe, milima, punda, mifupa mikavu na leso havina uhai kabisa havijiulizi wala havina udadisi na havina wasiwasi lakini imani iko juu kwa namna ambayo vinawezakutunza nguvu za Mungu hata kwa muda mrefu ulliokusudiwa pasipo kupoteza. Ona hapo juu kwa habari ya Paulo na wale watoto saba wa kuhani mkuu skewa walikuwa wanamjua Mungu na kanuni zake lakini mapepo yaliwashinda na kuwaumiza vibaya lakini cha kushangaza na ajabu kwelikweli vitambaa vilibeba nguvu ya Mungu vikaponya wagonjwa na kutoa mapepo hali havijui kitu, havisikii kitu wala havidadisi kitu lakini vilibeba nguvu ya Mungu na kwa maagizo ya Paulo vikatimiliza mpango wa Mungu kwa namna isiyochunguzika wala kuelezeka.

Hata Balaam nabii alipoambiwa akawalaani wanawaisraeli waliobarikiwa na Mungu punda alizungumza kumukumbusha kuwa Mungu ni waajabu huwezi kufanya kile ambacho hajakusudia kwa watu wake, hivyo punda alikuwa imani yake kuliko Balaam.

Kivuli ni kitu cha muda na cha kupita lakini kwa muda mfupi wa kuwepo kwake kilitunza nguvu za Mungu na kuponya wagonjwa, Je’sisi si zaidi ya hicho. Kuwa Mkristo sharti wasifu wa kristo usomeke ndani yetu ili tuweze kufanya zaidi ya mame, mifupa mikavu, vitambaa, vivuli vile vifanyavyo. Ufunuo 21:7-8 unatueleza namna ya kuwa mwana wa Mungu kweli. Pia wakorintho wa pili 10:5 inatusisitiza ili tudumu katika imani hii ya kristo tuangushe mawazo na kila kitu kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu na huku tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii kristo, Amina.

No comments:

Post a Comment