#SISI NI CHUMVI YA DUNIA

   Sukari huhitajika hata ikiwa yenyewe, na wengi huvutika kwa hiyo lakini si wengi waitakayo chumvi ikiwa yenyewe pasipo mchanganyiko. Ndio maana hata ikiwekwa sukari na chumvi huwezi kuta wadudu wamejaa na wengine kufa kwenye chumvi bali katika sukari. Hivyo chumvi huhitajika pale tu ikichakachuliwa au ukichanganywa na kitu kingine ambacho hakitokani na chumvi lakini si kwa sukari wengi huihitaji hata ikiwa yenyewe inavuta. Kuna usemi unasema eti “masugamami” jiulize kwa nini wasiwaitwe masaltimami haiji na kama wakiitwa hivyo na kuwepo wa aina hiyo hawahitajiki kwa wengi. Na ndio maana biblia katika (mathayo 5:13) inasema sisi ni chumvi ya dunia; hatujachakachuliwa na kama tukichakachuliwa hatufai tena kwa matumizi bali kuteketezwa katika moto. Yesu alimuita shetani kama mkuu wa dunia hii, na ndio maana yeyote ajaye duniani kwa mara ya kwanza kwa njia ya kuzaliwa kupitia wazazi lazima asajiliwe duniani kama mtu aliyekuja duniani na sio kama mtu aliyekuwapo duniani na asipofanya hivyo hana sehemu katika dunia wala hatambuliki na falme za duniani, kwa hivyo shetani anatapatapa sana na kutaka kujiinua kila iitwapo leo anahangaika na kushika kila idara ya dunia popote palipodhaifu kuanzia chini hadi katika level ya ufalme au uraisi. Na ndio maana kila kiumbe cha Mungu kijavyo duniani lazima atafute kukichakachua kabla hata ya wakati ulioamriwa ili kishikanane na dunia na anasa zake, lakini kwa sababu ya Neema ya Mungu iliyokatika Kristo Yesu hata atuchafuapo tangu kuzaliwa kwa namna ya mwili kutoka tumboni mwa mama zetu kuna kuzaliwa kwa mara ya pili ambako huko sio kwa namna ya mwili bali kwa namna ya rohoni ambapo huku kuna kushinda kushindako dunia yaani ile kuamini katika Kristo Yesu wa Nazareti kuwa ni mwana wa Mungu na Mungu kweli.

Hivyo tuzaliwapo mara ya pili kutokana na Roho Mtakatifu na tuwe chumvi ya kufaa isiyoharibika ili dunia ione kitu kipya kisichofananishwa au kuzoeleka kama ilivyo kwa vingine, kitu kilichochenyewe chenyewe na hiyo ndiyo chumvi halisi inayofaa na kuhitajika na BWANA wetu Yesu wa Nazareti, Amina.