Kama ilivyomtu akinyoa / kukata nywele huota na kukua tena au akikata
kucha hukua tena au akijikata ngozi kidonda kinafunga tena. Hivyo kila kitu
ndani yetu na nje ya miili yetu kinaongozwa na kulindwa Kiroho.
Ndivyo ilivyo kwa mtu ambaye Mungu amembariki, watu waweza fikiri
kuwa ni mwisho wako kwamba ndio umepotea lakini kumbe Mungu anakufanyia nguvu
mpya na unaanza kujawa na uweza kwa upya katika kila kitu.Tunaona kwenye kitabu
cha Waamuzi 16:19&22; Samsoni walipomnyoa nywele wakijua wamemaliza nguvu,
nywele zikakua tena na akaanza kuregain power pasipo wao kujua ndipo alipoomba
rehema kwa Mungu juu ya kujirudishia kisasi kwa maadui biblia inasema mauaji
aliyofanya wakati wa kufa kwake yaani maadui aliowaua wakati wa kufa kwake
walikuwa wengi zaidi kuliko aliowaua wakati bado yu hai. Mhubiri 11:5 inasema;
Kama vile wewe usipojua njia ya upepo ni ipi, wala jinsi mifupa ikuavyo tumboni
mwake mja mzito; kadhalika huijui kazi ya Mungu, afanyaye mambo yote. Na ndio maana katika Luka 1:26-27 Neno
linasema;“Mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa
Galilaya, jina lake Nazareti, kwa mwanamwali bikira aliyekuwa
ameposwa na mtu, jina lake Yusufu, wa mbari ya Daudi; na jina lake bikira huyo
ni Mariamu”. Unaona wakati Bikira Maria anafikilia kuolewa na kwamba asije
akaachwa na Yusufu, Malaika Gabriel alitumwa na Mungu kwake kwa habari Njema
tofauti na alivyokuwa anafikiria na pengine tofauti na alivyokuwa anaomba kwa
Mungu.
Ndugu, Mungu ndio anajua kwa kina yapi yatajiri kwetu, uwazavyo yaweza
kuwa siyo wala wakuwaziavyo pia yaweza kuwa sivyo Mungu ndio anampango mzima
kuhusu maisha yako soma Luka 12:22-34 ikutie nguvu. Sisi tunaongozwa na kulinda
na uungu wa Mungu kupitia roho wake Mungu, yeye ndiyo hufanya yote kwa nguvu
itendayo kazi ndani yetu, Ushawahi kujiuliza kwa nini saa nyingine ukiwa katika
kutaka kutenda jambo baya roho yako inasita au wakati jambo baya ambao
lingeweza kukupata ghafla rohoni unapata msukumo wa ajabu ambao kwa huo
unaepushwa katika ajali hiyo.
Ndugu! Mungu anakupenda yeye ni Mungu wa wote
wenye mwili wala si wakristo tu au watakatifu tu bali wa wote yaani hata
waislam, wapagani, wahindu, wachawi, wajambazi, na wote watendao maovu ni Mungu
wetu wote. Lakini kuna garantii ya pekee kuwa mwenye haki kwa maana hata Mfalme
Daudi katika zaburi 37:17; anasema ya kwamba tangu alivyokuwa kijana hadi
anazeeka hayawahi kuona mwenye haki wa Mungu ameachwa au amepatwa na baya au
Mungu kamsahaulia mbali na hata kizazi chake kuishi maisha ya shida kwa maana
ipo neema ya ajabu Mungu anapokuwa kimbilio lako Mfalme Daudi ameshuhudia kwa
nafsi yake akitendewa yaliyo mema na Baraka tele. Kuna raha ya ajabu wala
kuaibika hakupo kwao wamtegemeao Mungu utafanikishwa na kupitishwa sehemu
ambazo si kwa akili wala uweza au nguvu ndani yako na hata usingefikiri au kuwa
hivyo, lakini kwa kuwa na roho wa Bwana yu juu yako mambo makuu yatatendeka kwako.
Kwa habari ya kuhakikishiwa uzima, tunajua hakika walikuwepo wanabii wakubwa
wakapita na mitume wakubwa pia na hata watu washuhuri waliokuwa na uwezo hata
kulinda mataifa yao yasizuliwe wakapita hakuna hata mmoja aliyewahi kuahidi
kuwa atakuwa pamoja nao hadi utimilisho wa dahari isipokuwa YESU wa NAZARETI.
YEYE asema nitakuwa nanyi milele kwa hivyo tunamtegemea kwa sababu ana ahadi ya
milele inayothibitika hata katika maisha yetu ile Imani ni ushuhuda tosha ya
kwamba tunaye Mungu na ndio maana hata Ayubu 19:26 katika Biblia anasema hata
pasipo mwili huu NITAMWONA BWANA. Hivyo ushindi ni lazima, iwe katika mwili huu
au katika roho, Mungu katika Imani yako akupe ujasiri ndugu kushinda
yakushindayo. Be blessed, Amen!!
No comments:
Post a Comment