#USHUHUDA KUHUSU YESU WA NAZARETI NI NENO LENYE NGUVU

Ufunuo 12:11; Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana kondoo na kwa neno la ushuhuda wao.
Katika Biblia tunasoma ushuhuda wa Yohana mbatizaji kuhusu Kristo jinsi ulivyokuwa na nguvu (Yohana 1:19-23) mpaka akaulizwa je’ wewe ni kristo? au Nabii Eliya? akawaambia mimi sio! bali ni sauti ya mtu aliaye nyikani…… Angalia Yohana mbatizaji hakufanya ishara yoyote iliyopatwa kurekodiwa ndani ya biblia lakini Neno lenye nguvu lililotoka midomoni mwake lililojawa nguvu ya Mungu na roho wenye wasifu wa eliya nabii ndilo lililobadilisha hali ya hewa, mpaka watu kujisikia kusukwa sukwa mioyoni mwao. Neno lililochoma mioyo yao lile neno la Mungu ambalo alilikiri na kulishuhudia lililowafanya wengine wadhani ndiye Kristo hilo ndiyo Neno la USHUHUDA kuhusu Yesu wa Nazareti linachoma kama moto lawanyenyekeza hata wenye kiburi na wagumu wa mioyo?

Ndugu uliyeokoka na wengine mlio katika neema yake ya wokovu, maneno yako yawa nguvu na si bure ile sauti inayotoka mdomoni mwako katika ukiri na ushuhuda wa kristo na damu yake yanamaanisha kuwa kuna nguvu katika Neno la Mungu yaani Imani yako katika kristo Yesu inafanya maneno yako yasiwe maneno matupu bali yaliyojawa na roho mtakatifu. Ishara, maajabu na miujiza ni kwa kulainisha mioyo ya waliowagumu katika kumwamini Kristo na kumkubali kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yao na ya kwamba yeye kweli ndiye muumba wetu. Kama ukishakumwamini na kuwa na Imani naye huhitaji tena ishara, maajabu na miujiza bali baraka na mafanikio zaidi kumbuka Mtume Paulo anasema Mkubwa hahitaji tena maziwa bali walio wachanga Kiroho. Na ndio maana katika biblia Luka 10:20; Yesu wa Nazareti "lakini msifurahi kwa vile pepo wanawatii bali furahini kwa sababu majina yenu yameandikwa mbinguni.” hivyo si hayo mengine bali utakatifu na haki.

Yohana 10:41…inasema Yohana mbatizaji hakufanya hata ishara moja, lakini yote aliyoyasema ni kweli kuhusu ule USHUHUDA WA NENO AMBAYE NDIYE KRISTO, kwa hivyo Neno la Mungu ni ushuhuda na ni injili ya Yesu kristo na ni kweli (Luka 24:27) tukiamini. Katika Mathayo 11:21-24 Yesu anasema ole wenu Korazini na Bethsaida miujiza iliyofanyika kwenu ingelifanyika Tiro na Sidoni wangetubu kwa magunia na kwa kujipaka majivu na akasema Yesu itavumilika kwao kuliko ninyi. Alisema ole kwa Kapernaumu pia kwa ile miujiza aliyoifanya huko na akasema kama ingelifanyika Sodoma ingelibakia hadi hivi leo. Biblia inasema alisema ole wenu hizo sehemu kwa sababu alifanya miujiza mingi lakini mioyo yao iliendelea kuwa migumu na kutokumuamini, na ni kweli kuja kwa nuru kwetu au ile kweli ndiyo kuja kwa hukumu na haki ndio maana upinzani ni mkubwa kwa sababu hakuna aliye wa giza ufurahiaye hukumu na haki bali wa nuru. Hivyo ishara, ajabu na miujiza zatumika kama sumaku (yaani ni kama Biblia inavyosemea kuhusu kuvua watu kama inavyotokea katika uvuvi wa samaki na sehemu nyingine kwa wale waliokuwa na ulemavu, Yesu wa Nazareti alisema ni kwa ajili ya utukufu wa Mungu vile miujiza ilivyotendeka kwao); kwa hivyo yote hayo yalitendeka ili kumwamini Kristo, kisha kumsikia na kweli ipate kukaa ndani yetu tusipatwe kutikiswa na ufalme wa giza. Biblia pia inathibitisha katika Isaya 53:11 inasema kuwa …….kwa maarifa yake mtumishi wangu mwenye haki (Yesu) atawavuta wengi na kuwafanya wenye haki na kubeba madhaifu yao, lakini Neno lake; ule ushuhuda wake ndiyo kweli inoao na kuwafanya wengi wenye haki, na ndio maana biblia pia inasema kuhusu Yesu kwamba ;” Haijawahi kutokea mtu kuzungumza kwa mamlaka namna hii kama yeye” – Hivyo Neno lenye nguvu, la mamlaka, lijengalo, liumbalo, lifungalo na kufungua vitu, ndio msingi mkuu wa injili ya yesu kristo ya kwamba Ufalme wa Mungu uwe ndani yetu yaani ule Utatu mtakatifu ili dunia iweze kutawaliwa na kuongoozwa na nguvu ya Mungu utendayo kazi ndani yetu kupitia jina la Yesu kristo wa nazareti na siyo shetani wala utawala wa giza.

Tamka kwa nguvu; Sauti yangu ni nguvu za Mungu na ni mamlaka tosha dhidi ya shetani na ufalme wake katika jina la Yesu kristo wa nazareti, Amina.