#WAZAZI WALEENI WATOTO KATIKA NJIA YA KRISTO

Mithali 22:6 inasema; “mlee mtoto katika njia impasayo, naye
hataiacha, hata atakapokuwa mzee”. Hivyo ni malezi ndiyo yafanyayo
watoto kuwa wema au wabaya au watukutu, kumbuka huwezi
kuwatenga watoto na jamii, nchi au dunia hii iliyojaa yote mema na
mabaya isipokuwa kwa kuwajaza nguvu ya kushinda majaribu ya
dunia ambayo imo katika Neno la Mungu.
Kwa habari ya Ibrahimu anasemaje basi Bwana Yesu pale alipokuwa
akijiuliza amwambie au kumficha Ibrahimu kuhusu kusudi lake la
kuteketeza Sodoma na Gomora; Bwana anasema nimemjua ya
kwamba atawaamuru wanawe, nyumba yake baada yake waishike
njia ya Bwana, wafanye haki na hukumu (Mwanzo 18:19).
Kuhusu Mfalme Yoashi wa Israeli alianza kutawala tangu akiwa na
miaka 7 na alitawala miaka 40; Pale bibi yake yaani Athalia ambaye
alikuwa mtoto wa Ahabu and Yezebeli alipotaka kuwa Malkia
aliwauwa watoto wote wa Mfalme Ahazia mwanae, ambapo ni Yoashi
tu pekee alifanikiwa kutoroshwa na shangazi yake na kufichwa kwenye
chemba za hekalu akiwa bado mtoto mdogo na alifundishwa njia ya
haki ya Bwana na Kuhani Yehoyada kwa miaka 6 hekaluni alimofichwa
na akaielekea njia hiyo akafanya yaliyomema machoni pa Bwana kama
alivyofunzwa na kuhani, akatenda yaliyo ya haki na hukumu kipindi
chote cha ufalme wake (2 Wafalme 11:1-12; 12:1-2).
Pia Modekai aliyemulea Esta ambaye alikuwa yatima binti wa mjomba
wake, alimfundisha na kumkuza katika maadili mema, naye akaifuata
njia ya Bwana akawa mwanamke mwema na mwadilifu naye akayaishi
yote, akatenda haki na hukumu na mwishowe akaiponya Israeli na
maangamizo yaliyokuwa yamekusudiwa kwa hila na Hamani (Esta 2:7).
Kuhani Eli hakuwaonya watoto kuhusu kuielekea njia ya haki laana
ikaifuata familia na uzao wake ukaangamia naye Eli pia (1 Samweli
2:12; 3:13-14).
Lutu aliishi nchi ya anasa ya sodoma na gomora lakini kutokana na
kutowanyoosha watoto wake njia ya haki, pamoja na kuponywa na
Bwana na kiama ya moto; bado wanawe dhamiri na nafsi zao
zilishikamana na yale yaliyokuwa yakitendeka sodoma na gomora,
hawakushikimana na njia ya haki nao wakazini naye akiwa amelewa
na kuzaa watoto wa kiume na baba yao na habari yake Lutu ikaishia
hapo (Mwanzo 19:1-38).
Hata Paulo alitambua suala la malezi ya imani lilivyo na muhimu,
pale alipomwambia Timotheo (2 Timotheo 1:5-6); "nikiikumbuka imani
uliyonayo  isiyo na unafiki, ambayo ilikaa kwanza katika bibi yako Loisi,
na katika mama yako Eunike, nami nasadiki wewe nawe unayo. kwa
sababu hiyo nakukumbusha, uichochee karama ya Mungu, iliyo ndani 
yako kwa kuwekewa mikono yangu".
Hivyo ndugu ishike njia ya haki wewe na nyumba yake yote kwa
maana hakika zimwi likujualo halikuli likakwisha hivyo suluhu ni Neno
la Mungu likae kwa wingi ndani yetu na kwa watoto wote kwani
hakuna njia ya kupingana na shetani na ufalme wake isipokuwa kwa
kuwa karibu sana na Mungu ile imani yako.
Wazazi tujifunze na tuwe kama Yohana mbatizaji, tuiandae njia ya
Bwana katika familia zetu ili watoto wamuishe yeye Kristo na siyo
kuvutwa na anasa za dunia ambalo ni pando la adui shetani, yaani
awakute wakiwa wameandaliwa nakujua Bwana Yesu hakika ndiye
Mungu.
Kwa maana kama wana wa Lutu wangemjua Mungu yaani njia ya
kweli na haki ile dhambi ya sodoma na gomora isingewafutilia mpaka
kule kwenye makao mapya. Kwa hivyo suluhu nikuwa na nguvu ya
Neno la Mungu kumshinda shetani ili awaonapo awakimbie; kwa
maana ni kwa Neno la Mungu lililojaa ndani yetu tunampinga shetani.
Kumbuka kushindana na shetani ni kushindana na ufalme wa giza
tunapingana nao, kwani pepo akitoka huyu anakuja huyu kwa hivyo
suluhu ni moja tu we jaza Neno la Mungu ndani ambalo ndiyo Mungu
mwenyewe; yaani Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho
Mtakatifu na hilo ndilo litakalomuweka shetani na ufalme wake mbali
nao. Ndiyo! Neno la maarifa, Biblia inasema tunaangamia kwa kukosa
maarifa, na maarifa ni katika Neno la Mungu.

Sala; Mwenyezi Mungu niongoze mimi kama mzazi kwa neema yako
niweze kuwalea watoto wangu katika njia iwapasayo iliyo ya Haki ya
Bwana nipe hiyo karama Bwana Yesu ili wadumu katika kweli na
mioyo minyofu siku zote za maisha yao katika jina la Yesu Kristo wa
Nazareti, Amina.

No comments:

Post a Comment