Monday, October 28, 2024
#KINGDOM WAY (TEMPLE, U)
Tuesday, October 15, 2024
#UFALME WAKE, UFALME WETU
Luka 12:29-32 inashangaza sana, Yesu anasema; "Msiogope! enyi kundi dogo, kwa kuwa Baba yenu ameona vyema kuwapa nyie huo Ufalme". He said; "It's your Father's good pleasure to give you the Kingdom." Hata Daniel 7:27 alitabiri kwa habari ya wana wa Mungu akisema; "Na ufalme, na mamlaka, na ukuu wa ufalme, chini ya mbingu zote, watapewa watu wa watakatifu wake Aliye juu; ufalme wake ni ufalme wa milele, na wote wenye mamlaka watamtumikia na kumtii".
Tena katika Yohana 17:22 Yesu anasema; "Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao; ili wawe na umoja kama sisi tulivyo na umoja". ona He said; "that glory which you gave me, i have given them", this is powerful!
Sikia hii; aliteswa tupate haki ya kuwa na kuitwa wana wa Mungu.
Iliyoitwa kufuru kuwa mwana wa Mungu ikawa haki yetu.
Kwa uthubutu wake, akagharamia hata mauti yake, alitamka hivyo ikawa.
Na haki hiyo ilikuja na uweza uliotupa sisi ujasiri na nguvu katika ukiri wetu kuwa sisi ni wana wa Mungu hakika.
Ilimchukua yeye kuishi kama sisi ili tuupate ufalme wake (Wafilipi 2:6-8); yeye mwenye namna ya Mungu toka mwanzo alichukua namna ya mtumwa akawa na mfano wa wanadamu halafu alijinyenyekeza sana akawa mtii mpaka mauti, naam, mauti ya msalaba (kwani ilikuwa laana mtu kuangikwa msalabani-Wagalatia 3:13-14), Yesu anasema jina lako Baba litukuzwe duniani (Yohana 12:28, 17:4,6), kwamba kuitwa kwetu sisi wana wa Mungu ni utukufu kwa Mungu Baba.
Fikiria jina lake la heshima Yesu; imeandikwa ktk Wafilipi 2:9-11 kwa jina hilo kila goti lipigwe la vitu vyote vya mbinguni, duniani na kuzimu.
Halafu, alizaliwa nalo kikawaida kabisa, kipindi kingine alikimbizwa nalo kwenda kufichwa Misri, aliishi nalo mitaani, wakati mwingine hata hakujilipizia nalo pale watoto wenzake walipomuonea, kuna kipindi akiwa mdogo aliwachallenge nalo walimu wa sheria Yerusalemu hawakumtambua vizuri alivyo mwana wa ahadi na hatima, alicheza nalo na hakuna aliyejua, saa ilipofika akajifunua kwalo hakuna aliyemsadiki, alikataliwa nalo, akatukanwa nalo, akatengwa nalo, balaza kuu la makuhani (Sanhedrin) likamuhukumu nalo (Isaya 53), ngoja nikuambie hivi, daraja la ukuhani liliikumbatia laana ya torati, lile lililokuwa njia kumfikia Mungu kama ilivyokuwa kanuni yake Mungu likageuka kifungo, kizuizi kwa watu kumfikia, sababu Mungu alipitisha hilo alipoitoa torati kwa mkono wa Musa akamfanya Haruni kama kuhani wa kwanza kuwakilisha watu wake wanisraeli patakatifu pa patakatifu na sasa Yesu aliwaita makuhani wale walimu wa sheria; mafalsayo na masadukayo kuwa ni kama majeneza yaliyopaka chokaa nyeupe nje huku ndani imejaa mifupa mitupu kwa vile walivyowabebesha watu mzigo mzito wasiyothubutu kuibeba wao, wakiwazuia watu kuingia patakatifu pa patakatifu na huku nao wamepoteza haki ya kupafikia. Hivyo kuhani mkuu Caiaphas hata alipomnyoshea kidole cha hukumu Yesu kumuapisha kwa jina la Bwana, Mungu anayeishi alilokuwa nalo yeye pasipo wao kulijua, kama ni kweli yeye ni mkombozi na mwana wa Mungu, kwa jina hilo akajibu; Ndiyo!, na kukiri kuwa karibu anaenda kwa Baba na karibu mwana wa Mungu atavikwa nguvu na kutawala tena wenyeji wote wa mbinguni, Kuhani mkuu kwa hasira kuu akararua vazi lake na kusema ni kufuru kubwa hii wala haihitajiki ushuhuda mwingine juu ya hukumu yake na hivyo wakamtesa sana nalo, na hata Pilato aliposema sina hatia juu ya damu ya mtu huyu, naona mmekusudia afe nami sijaona kosa juu yake, lile kundi (mob) likiongozwa na kuhani mkuu na makuhani wa Sanhedrin na masadukayo na wamafalsayo wakapiga kelele asulubiwe, na kisha wakasema na damu yake iwe juu yetu sisi na vizazi (watoto) vyetu, akasulubiwa nalo, akafa nalo msalabani na kuzikwa nalo. Haki yetu ya uwana wa Mungu ilipatikana pale golgotha kwa kumwagika damu yake Yesu ktk mauti ya msalaba, na kwa hiyo alituweka huru na dhambi, na hata pazia la hekaluni lilipasuka vipande viwili ili kwa ile haki ya uwana kwa kila anayemwamini aweze ingia patakatifu pa patakatifu binafsi azungumze na Mungu kama ilivyokuwa mpango wake wa awali toka enzi za Adamu.
Unaona kwa hiyo yaliyofanyika yote hayo, kwa ajili yako wewe na mimi, kwani hakuwa tayari kuona sisi tunanyanyaswa kwa kuwa gizani kuishi isivyotusitahili asili yetu, kwa hivyo siku ya tatu akafufuka nalo, halelujah! ili tu sisi tukamilishwe kwalo, tuitwe na tuishi kama wana wa Mungu, wana wa ufalme wa mbinguni duniani. Bwana Yesu Kristo asifiwe! ni habari njema sana hii..
Hivyo chukua nafasi hiyo sasa katika jina la Yesu Kristo wa Nazareti, pokea huo ufalme wa Mungu, kaa hapo ee! mwana wa Mungu, angaza nuru yake, barikiwa, occupy till when He come again. Indeed; you are the son/daughter of God, and when you are the son/daughter of God in Him you are sin-free, amen.
Saturday, October 12, 2024
#THE TRUTH CO-ORDINATED LIFE
Truth co-ordination among brethren complete the mind of christ in us. Living the truth co-ordinated life perfect our righteousness in God.
~1 Corinthians 2:16🙏
Tuesday, October 8, 2024
#HABARI NJEMA KWAKO!
Make Holy Spirit count on you,
Jesus Christ proud,
The Almighty Father smile and,
All the Heavens rejoice.
It's New Dawn now.
Thanks God 🙏🏾.
*Kukuwa katika imani ni pamoja na kutochanganyikiwa ktk semi hizi mbili👇🏾 kwa maana Kiti cha Enzi ni kimoja na Mungu aketiye juu yake ni mmoja tu, Baba wa Mbinguni*
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Mfanye Roho Mtakatifu awe nawe 🫵🏾,
Yesu Kristo aone fahari,
Baba mwenye enzi yote atabasamu,
nazo mbingu zikufurahie.
Ni mwanzo mpya,
Mshukuru Mungu.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Mfanye Roho Mtakatifu katika jina la Yesu Kristo aone fahari kuwa nawe,
yaani, Baba mwenye enzi yote atabasamu katika utukufu wake,
nazo mbingu zikufurahie.
Ni mwanzo mpya,
Mshukuru Mungu.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Ok!, ni kama kusema kwa mfano mzee mmoja mbobezi katika tukio la mafanikio ya mwanae katika uhasibu wake baada ya kusikia na kuona matukio yake ya kipindi chote ktk video, huku akiwa na moyo wa furaha alipopewa mic aseme neno akashusha pumzi kubwa na kusema;
"Hakika kwa roho wewe ni roho yangu kweli kweli ni ndani yako mimi, kama mhasibu mi pia, najivunia sana wewe na kama Baba nimefurahi na kufarijika sana kwa mafanikio yako, na boma yetu yote wafurahi na kuwa na shangwe kuu kwa ajili yako, ni mwanzo wako mpya tena huu nishukuru sana mimi. Ni mimi Yoshua."
Ni Habari njema?,
Ndiyo! ni njema kweli hizi🙏🏾
Thursday, October 3, 2024
#HOLY GHOST [ROHO MTAKATIFU]
God's Way not mere talk, it's an empowered life; living by God's power.
Ndio!, Ufalme wa Mungu ni nguvu ktk matendo na sio maneno sana (power in action)~1Wakorintho4:20.
Matendo 19:1-20; Neno la Mungu la ufalme (kingly word of God) lilizidi kuenea Efeso na kushinda kwa nguvu, sababu ya nini? uthihirisho wa Roho Mtakatifu.
Sasa kama ni majivuno kwa mkristo yeyote, ni kwa sababu ya kumpata Roho Mtakatifu, ambayo ni neema kubwa sana. Waliomsikia Yohana mbatizaji Neno linasema waliamini neno la toba wakatubu na kubatizwa ikaishia hapo, ila ktk Yohana 1:12 kwa waamini wote wa Yesu kristo Mnazareti, aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ule uwezo ndio nguvu iletwayo na Roho Mtakatifu.
Na je' sasa we ni mwamini wa Yohana Mbatizaji ama wa Yesu Kristo wa Nazareti? Jiulize!
Mwana wa Mungu kama kweli ndiye, son/daughter of God, omba uwe na Roho Mtakatifu, hapo inaleta maana ktk imani yako, na asiwe anaheri mpagani kukuzidi, naye huyo Roho akiwemo ndani yako atajithihirisha nawe utakiri kweli sasa ninaye.
Mfano mzuri ktk kizazi chetu mwanzoni mwa miaka ya 1900s, Mwafrika mweusi William J. Seymour, mtumishi wa Mungu huyu aliyekuwa kipofu jicho moja hakupendezewa na imani butu, alitamani matendo ya mitume yaendelee na aliamini kuwa kunena kwa lugha ni ishara mojawapo ya mtu kumpokea Roho Mtakatifu (Holy Spirit Baptism), akawa na shauku sana kila akisoma Matendo 2:4, shauku hiyo ikampelekea kuwa na mzigo kutaka kupokea na hata baada ya imani kujaa aliokuwa akiwahubiria wakaanza kupokea na kisha naye akajazwa Roho Mtakatifu miaka ya 1914, na ndio ulipozaliwa uamusho wa Roho mtakatifu kwenye mitaa ya Azusa ya Marekani, mpaka mitaani watu wakawa wanajazwa wanalewa Roho Mtakatifu na kuanza kunena kwa lugha mpya, na huo ukawa mwanzo mpya tena wa upentekoste kuenea kwa kasi baada ya kanisa kupoa kwa muda na huduma nyingi zikaanza utume duniani kama Assemblies of God iliyoenea duniani kwote, nawe unajua kama hapa Tanzania huwezi zungumzia mwanzo wa upentekoste bila kutaja Tanzania Assemblies of God (TAG), lakini jua ilianza na shauku ya mtu mmoja, hii ikithibitisha kuwa Mwana wa Mungu kweli akiwa na Roho Mtakatifu ni Kuhani wa Kifalme na Taifa teule🙏🏾.
so,
#Receive Holy Spirit
#Live like King, talk like Him
#Kingly virtues.
#Serve the Almighty God