Tuesday, January 28, 2025

#MWAKA WA KUONA _2025


 KUONA KUKUPAKO KUSHINDA

Wangapi wanajivuna kwamba Naona!! Mikono juu! (Kwa maana Yesu anasema nalikuja kwa hukumu ili wanaosema wanaona wawe vipofu na vipofu waone- Yohana 9:39), safi!!, Sasa 2025 sema "Nitatazama, Nitaona"...,  Nami nakuombea; nguvu ya kuona iongezeke ndani yako leo, kama mi niitajivyo.

Unajua ukisoma Luka 11:34 inasema; "Jicho lako ni nuru ya mwili wako. Macho yakiwa mazima huangaza mwili wako wote; lakini yakiwa mabovu, mwili wako pia utakuwa katika giza". This means pasipo kuona no direction!..

Jifunze kwa Bathromeo kuona kuna baraka kuu sana, tamani kuona, nasema tena tamani kuona (Marko 10:46-52).

Ng'ang'ana mpaka uone mwaka huu;

Wengi wanatazama, wanapepesa macho, wanaangalia lakini hawaoni, mtu awaye yote asikudanganye, kuna kuona, kuna kuangalia ni tofauti, kuona kunafaida sana, kunakupa maamuzi sahihi, kunakupa amani, kunakukombolea wakati, kunakupa kufikia malengo kwa muda mwafaka, kunayapa maisha maana, mtu anayeona anafocus ya maisha..

Hata ukisoma tena Marko 8:22-25 kuna kipofu yule wa Bethseida alipokuwa anawezeshwa na Yesu kuona akasema naona kama miti inatembea, kisha akamuwekea tena mikono machoni, ndipo alipotazama sana ule umakini ktk kutazama akaona vyote waziwazi!! (yaani ile live bila chenga). Unajua nini pasipo juhudi za kutaka kuona clear huwezi kuona, Roho wa Bwana yupo nasi yupo karibu yako ulipo, tamani sasa, nasema tamani sasa kuona, uone....

Kwenye Biblia, Yeremia anaulizwa  na Mungu, UNAONA NINI? mara aseme nimeona hiki mara nimeona kile, na alipoona Mungu akamwambia UMEONA VYEMA. (Yeremia 1:11-12). Kule kuona kuna matokeo yake, na hata Bwana akasema ninaliangalia neno langu ili nilitimize, ni kwa namna utavyoona.

Kuna kuangalia na kuona. Na ni baada ya kuangalia huja kuona. For you can't have step by looking until you see.

Sasa, its only what you see that which you can get, than what you are looking at. The mind is not settled in looking but in seeing, yaani; ni kile tu utachokiona ndicho utaweza pata, kuliko unachoangalia hapo hata akili inakuwa haijakupata na ufahamu hauwezi kukupa chochote cha kutamkwa yaani wazo ili kiumbike kwako. Kwani ni kweli unaweza ukaangalia na usione na akilini usipate kitu, lakini ulichokiona, ulishakiangalia na mind said something on that, na hakika utakipata. Unapoona ufahamu unawajibika, unapoangalia ufahamu haujui kitu bado.

Unaona pia pamoja na kumsikia Bwana, kule kuweza kuona ile ishara ya kijiti kilichowaka moto bila kuteketea, kulimpa mungu Musa aliyekuwa zaidi ya nabii uhakika na hatua, na ndipo aliweza kuwa na ujasiri wa kumuelezea Mungu kwa taifa la Israeli kule Misri pasipo hofu na hatimaye kumshinda Farao na jeshi lake lote (Kutoka 3: 2-4).

Mwamuzi Gedioni pamoja na kuonekaniwa na malaika wa Bwana na ishara ya sadaka kulambwa na moto wa mbinguni. Lakini ili awe na hakika wa kulikabiri lile jeshi kubwa la wamidiani na waamaleki waliokuwa kama mchanga wa bahari, alitaka aone ishara zaidi (Waamuzi 6:36-40), zimupe uhakika, nguvu na ujasiri, pamoja na kwamba kusikia neno la ushindi kuliipa nguvu mkono yako kwa vita, alihitaji kuona ishara zaidi za Mungu.

Unaona pia, ujasiri wa Gehazi haukutokana na kumwamini nabii Elisha sababu alikuwa bado na shaka pale jeshi kubwa la washami la mfalme Ben-hadadi lilipowazingira Israeli yote, wala haukutokana na miujiza ama ishara nyingi za Mungu zilizofanyika kupitia mkono wa bwana wake Elisha, la hasha! bali saa zile tu alipoweza kuona jeshi la malaika wa mbinguni ndipo aliposadiki sawa sawa (2 Wafalme 6:8-23).

Hivyo nawe utachokiona sasa kikufanye kuwa jasiri zaidi na uhakika zaidi, ili hatua kuu ukaiishi, nawe ukawe mshindi, nayo ahadi ya Mungu ikafanyike halisi kwako. Nguvu ya kuona iongezeke ndani yako uyaishi hayo maono, na sio kile wanachokuambia watu kuwa ndicho bali kile utachokiona kiishi hicho, amini katika hicho mpaka kitimie.

Kunacases mbili kwenye Biblia, zinazoonyesha namna takwa la kuona linaweza timizika, and that is our prayer point now. 

-> Isaya 6:1-3 anasema katika mwaka ule aliokufa Mfalme Uzia nalimwona Bwana ameketi katika kiti cha enzi,....

-> Alipotengana na Lutu tu, MUNGU akamwambia Abramu inua macho tazama/ANGALIA pande zote, nchi hii ULIYOIONA nitakupa wewe na uzao wako hata milele. Ondoka ukatembee katika nchi hii kwa marefu yake na mapana yake, maana nitakupa wewe nchi hii (Mwanzo 13:14-17).

Hitimisho:

Ahadi ni kweli ya kwamba, KWA NAMNA UTAVYOWEZA KUONA, that's means you need to strive to see crystal clear, anasema NITAKUPA WEWE NA UZAO WAKO, kuna sharti ndani ya neno so, ni lazima uyatende mapenzi ya Mungu, akipendezwa nawe hakuna kitakachozuia kukipata alichoahidi. Amina.

No comments:

Post a Comment