Thursday, October 3, 2024

#HOLY GHOST [ROHO MTAKATIFU]


God's  Way not mere talk, it's an empowered life; living by God's power.

Ndio!, Ufalme wa Mungu ni nguvu ktk matendo na sio maneno sana (power in  action)~1Wakorintho4:20.

Matendo 19:1-20; Neno la Mungu la ufalme (kingly word of God) lilizidi  kuenea  Efeso na kushinda kwa nguvu, sababu  ya  nini? uthihirisho wa  Roho  Mtakatifu. 

Sasa kama ni majivuno kwa mkristo yeyote, ni kwa  sababu ya kumpata Roho  Mtakatifu, ambayo ni neema kubwa sana.  Waliomsikia Yohana  mbatizaji Neno linasema  waliamini neno la  toba wakatubu na  kubatizwa ikaishia hapo, ila ktk  Yohana 1:12 kwa waamini  wote wa Yesu kristo Mnazareti, aliwapa uwezo  wa   kufanyika watoto wa  Mungu,  ule  uwezo ndio nguvu iletwayo na Roho  Mtakatifu.

Na je' sasa we ni  mwamini wa  Yohana  Mbatizaji ama wa Yesu Kristo wa Nazareti?  Jiulize!

Mwana wa Mungu kama  kweli ndiye,  son/daughter of God, omba uwe na Roho  Mtakatifu, hapo  inaleta maana ktk imani yako, na asiwe anaheri   mpagani kukuzidi, naye  huyo Roho akiwemo ndani yako atajithihirisha nawe utakiri kweli sasa ninaye.

Mfano mzuri ktk kizazi  chetu  mwanzoni mwa miaka ya 1900s, Mwafrika  mweusi  William J.   Seymour, mtumishi wa  Mungu huyu aliyekuwa  kipofu jicho  moja hakupendezewa na imani butu, alitamani  matendo ya  mitume yaendelee na aliamini kuwa kunena kwa lugha ni ishara mojawapo ya  mtu  kumpokea Roho  Mtakatifu (Holy  Spirit Baptism), akawa na  shauku sana kila  akisoma  Matendo 2:4, shauku hiyo ikampelekea kuwa na  mzigo kutaka kupokea na  hata  baada ya imani  kujaa aliokuwa  akiwahubiria wakaanza kupokea na kisha naye  akajazwa Roho Mtakatifu miaka ya  1914, na ndio ulipozaliwa uamusho wa Roho   mtakatifu  kwenye  mitaa ya  Azusa  ya Marekani, mpaka mitaani  watu wakawa  wanajazwa wanalewa  Roho Mtakatifu na kuanza kunena  kwa lugha  mpya, na huo  ukawa  mwanzo mpya tena wa upentekoste  kuenea  kwa  kasi baada ya kanisa  kupoa kwa muda na huduma nyingi zikaanza utume duniani kama Assemblies of God iliyoenea duniani kwote, nawe unajua kama hapa Tanzania  huwezi zungumzia mwanzo wa  upentekoste bila kutaja Tanzania Assemblies  of God (TAG), lakini jua ilianza na shauku ya mtu  mmoja,  hii ikithibitisha  kuwa Mwana  wa Mungu kweli  akiwa na Roho Mtakatifu ni Kuhani wa Kifalme na Taifa  teule🙏🏾.

so,

#Receive Holy Spirit

#Live like King, talk like Him

#Kingly virtues.

#Serve the Almighty God

No comments:

Post a Comment