Tuesday, October 15, 2024

#UFALME WAKE, UFALME WETU

Luka 12:29-32 inashangaza sana, Yesu anasema; "Msiogope! enyi kundi dogo, kwa kuwa Baba yenu ameona vyema kuwapa nyie huo Ufalme". He said; "It's your Father's good pleasure to give you the Kingdom."

Hata Daniel 7:27 alitabiri kwa habari ya wana wa Mungu akisema; "Na ufalme, na mamlaka, na ukuu wa ufalme, chini ya mbingu zote, watapewa watu wa watakatifu wake Aliye juu; ufalme wake ni ufalme wa milele, na wote wenye mamlaka watamtumikia na kumtii".
Tena katika  Yohana 17:22 Yesu anasema; "Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao; ili wawe na umoja kama sisi tulivyo na umoja".  ona He said; "that  glory which  you gave me, i  have given them", this is  powerful!
Sikia hii; aliteswa tupate haki ya kuwa na kuitwa wana wa Mungu.
Iliyoitwa kufuru kuwa mwana wa Mungu  ikawa haki yetu.
Kwa uthubutu wake, akagharamia hata mauti yake, alitamka hivyo ikawa.
Na haki hiyo ilikuja na uweza uliotupa sisi ujasiri na nguvu katika ukiri wetu kuwa sisi ni wana wa Mungu hakika.

Ilimchukua yeye kuishi kama sisi ili tuupate ufalme wake (Wafilipi  2:6-8); yeye mwenye namna ya  Mungu  toka  mwanzo alichukua namna ya  mtumwa akawa na mfano wa  wanadamu halafu alijinyenyekeza sana akawa mtii mpaka mauti, naam, mauti ya msalaba (kwani ilikuwa laana mtu kuangikwa msalabani-Wagalatia 3:13-14), Yesu anasema jina lako Baba litukuzwe duniani (Yohana 12:28, 17:4,6), kwamba kuitwa kwetu sisi wana wa Mungu ni utukufu kwa Mungu Baba.
Fikiria jina lake la heshima Yesu; imeandikwa  ktk Wafilipi 2:9-11 kwa jina hilo kila goti lipigwe la vitu vyote vya mbinguni, duniani na kuzimu.
Halafu, alizaliwa nalo kikawaida kabisa, kipindi kingine alikimbizwa nalo kwenda kufichwa Misri, aliishi nalo mitaani, wakati mwingine hata hakujilipizia  nalo pale watoto wenzake walipomuonea, kuna kipindi akiwa mdogo aliwachallenge nalo walimu wa sheria Yerusalemu hawakumtambua vizuri alivyo mwana wa ahadi na hatima, alicheza nalo na hakuna aliyejua, saa ilipofika akajifunua kwalo hakuna aliyemsadiki, alikataliwa nalo, akatukanwa nalo, akatengwa nalo, balaza kuu la makuhani (Sanhedrin) likamuhukumu nalo  (Isaya 53), ngoja nikuambie hivi, daraja la ukuhani liliikumbatia laana ya torati, lile lililokuwa njia kumfikia Mungu kama ilivyokuwa kanuni yake Mungu likageuka kifungo, kizuizi kwa watu kumfikia, sababu Mungu  alipitisha hilo alipoitoa torati  kwa mkono wa  Musa  akamfanya Haruni kama kuhani wa kwanza  kuwakilisha watu wake  wanisraeli patakatifu  pa patakatifu na sasa Yesu aliwaita makuhani wale walimu wa sheria; mafalsayo na masadukayo kuwa ni kama majeneza yaliyopaka chokaa nyeupe nje huku ndani imejaa mifupa mitupu kwa vile walivyowabebesha watu mzigo mzito wasiyothubutu kuibeba wao, wakiwazuia watu kuingia patakatifu pa patakatifu na huku nao wamepoteza haki ya kupafikia. Hivyo kuhani mkuu Caiaphas hata alipomnyoshea kidole cha  hukumu  Yesu kumuapisha kwa  jina la Bwana, Mungu anayeishi alilokuwa nalo yeye pasipo wao  kulijua, kama ni kweli yeye ni mkombozi na mwana wa Mungu, kwa  jina hilo akajibu; Ndiyo!, na kukiri kuwa karibu anaenda kwa Baba na karibu mwana wa Mungu atavikwa nguvu na kutawala tena  wenyeji  wote wa mbinguni, Kuhani mkuu kwa hasira kuu akararua vazi lake na kusema ni kufuru  kubwa hii wala haihitajiki ushuhuda mwingine juu ya hukumu yake na hivyo wakamtesa sana nalo, na hata Pilato aliposema sina hatia juu ya damu ya mtu huyu, naona mmekusudia afe nami sijaona kosa juu yake, lile kundi (mob) likiongozwa na kuhani mkuu na makuhani  wa Sanhedrin na masadukayo na wamafalsayo wakapiga kelele asulubiwe, na kisha  wakasema na damu yake iwe juu yetu sisi na vizazi (watoto) vyetu, akasulubiwa nalo, akafa nalo msalabani na kuzikwa  nalo. Haki yetu ya uwana wa Mungu ilipatikana  pale golgotha  kwa kumwagika damu yake Yesu  ktk mauti ya msalaba, na kwa hiyo alituweka huru na dhambi, na hata pazia la hekaluni lilipasuka vipande viwili ili kwa ile haki ya uwana kwa kila anayemwamini aweze ingia patakatifu pa patakatifu binafsi azungumze na Mungu kama ilivyokuwa mpango wake wa awali toka enzi za Adamu.
Unaona kwa hiyo yaliyofanyika yote hayo, kwa ajili yako wewe na mimi, kwani hakuwa tayari kuona sisi tunanyanyaswa kwa kuwa gizani kuishi isivyotusitahili asili yetu, kwa hivyo siku ya tatu akafufuka nalo, halelujah! ili tu sisi tukamilishwe kwalo, tuitwe na tuishi kama wana wa Mungu, wana wa ufalme wa mbinguni duniani. Bwana Yesu Kristo asifiwe! ni habari njema sana hii..
Hivyo chukua nafasi hiyo sasa katika jina la Yesu Kristo wa Nazareti, pokea huo ufalme wa  Mungu, kaa hapo ee! mwana wa Mungu, angaza nuru yake, barikiwa, occupy till when He come again. Indeed; you are the son/daughter of God, and when you are the son/daughter of God in Him you are  sin-free, amen.

No comments:

Post a Comment