#KINGA YA KIROHO [ST. PATRICK BREASTPLATE]

Najiunganisha leo
/Na nguvu za Uungu, sala ktk utatu mtakatifu wa Mungu
/Na imani katika utatu wa Mungu
/Na ushuhuda wangu wa Muumba wa vyote

Najiunganisha leo
/Na nguvu ya kristo ktk kuzaliwa na ubatizo wake
/Na nguvu ya kristo ktk mateso ya msalaba na kifo chake
/Na nguvu ya kristo ktk Ufufuo na kupaa kwake
/Na nguvu ya kristo ktk kuja kwake kwa hukumu ya mwisho


Najiunganisha leo
/Na nguvu ya upendo wa makerubi wa Mungu
/Na utii wa Malaika zake Mungu
/Na huduma za Malaika walinzi wakuu
/Na matumaini ya ufufuo na kukutana na ujira wangu ktk Bwana
/Na sala za Washindi wa Imani waliotangulia
/Na utabiri wa Manabii wa Mungu
/Na Mahuburi ya Mitume wa Yesu kristo
/Na imani ya mashuhuda wa kristo Yesu
/Na mabikira watakatifu wasio na hatia
/Na matendo mema ya wenye haki


Najiunganisha leo
/Na nguvu za Mbinguni
/Na mianga ya jua
/Na mng’ao wa mwezi
/Na utukufu wa moto wa roho mtakatifu
/Na mwendokasi wa muwako wa mwanga
/Na mwendokasi wa mvumo wa upepo
/Na kina cha bahari
/Na msimamo wa dunia pasipo kutikisika
/Na mshikamano wa miamba


Najiunganisha leo
/Na nguvu za Mungu kuniongoza mimi
/Na uungu wa Mungu kunisaidia mimi
/Na hekima za Mungu kunilinda mimi
/Na macho ya Mungu kuniangalia mimi
/Na masikio ya Mungu kunisikia mimi
/Na Neno la Mungu kuongea badala yangu
/Na mkono wa Mungu kunishika mimi
/Na Ngao ya Mungu kunikinga mimi
/Na jeshi la Malaika zake Mungu kuniokoa mimi
/Kutoka ktk mitego ya mapepo wabaya
/Kutoka ktk matamanisho ya wasaidizi wake shetani
/Kutoka ktk kila mtu anitakiae ugonjwa awe wa mbali au karibu.


Najikusanyia mimi mwenyewe leo
/Mamlaka na nguvu zote hizi kati yangu dhidi ya hao mapepo wabaya
/Kinyume na kila nguvu ya shetani iharibuyo, ambayo yapinga mwili na nafsi yangu
/Kinyume na maneno ya kichawi ya manabii wa uongo
/Kinyume na sheria za giza za tawala za kipagani
/Kinyume na sheria za uongo za wapinga kristo
/Kinyume na waabudu sanamu
/Kinyume na ndumba za wenye nguvu za giza, waundao sanamu na wachawi
/Kinyume na kila elimu iharibuyo mwili na nafsi ya mtu
/Yesu Kristo nikinge mimi leo
/Kinyume na sumu, kinyume na kuungua moto wa kipepo, kinyume na kufunikwa na nguvu za giza, kinyume na majeraha ya roho, nafsi na mwili
/Ili yakwamba kwa hayo uje kwangu wingi wa ujira kutoka kwako bwana.         
 /Iwe ni kwa nguvu na kwa mamlaka ya yesu ktk roho mtakatifu.

Kristo na mimi
Kristo kabla yangu
Kristo nyuma yangu
Kristo ndani yangu
Kristo chini yangu
Kristo juu yangu
Kristo upande wangu wa kulia
Kristo upande wangu wa kushoto
Kristo nilalapo chini
Kristo nikaapo chini
Kristo nisimamapo
Kristo ktk moyo wa kila anifikiriaye mimi
Kristo ktk mdomo wa kila aniongeleaye mimi
Kristo ktk kila jicho linionalo mimi
Kristo ktk kila sikio linisikialo mimi


Nasimama leo
/Kupitia nguvu za uungu,maombi ktk utatu mtakatifu wa Mungu
/Kupitia imani katika utatu wa Mungu
/Kupitia ushuhuda wangu wa Muumba wa vyote
/Yesu kristo! yesu kristo!

JESUS! Ameeeeeeeeeeeeeeeen!!

1 comment:

  1. Barikiwa sana mtoto wa MUNGU roho mtakatifu azidi kukufunulia mengi zaidi

    ReplyDelete