Sunday, August 25, 2024

#U MWANA WA MUNGU

 


Somo  la  Yesu kwetu ni nini?

Uwana wa Mungu ni uwakilishi  wa Mungu Baba aliyeketi ktk kiti cha enzi, kama yeye alivyo mbinguni  ndivyo nasi tulivyo  duniani (Wakolosai 2:9-10, Waebrania 1:1-10).

Na usiwe na shaka kuhusu hili kwani kuna haki hiyo (Yohana 1:12-13).

Sasa ktk Mathayo 16:13-20; pale kaisaria-filipi ndipo ilifika hatua na saa ile ya Yesu kufunuliwa kama mwana wa Mungu ambao huo ufunuo ndio mwamba wenyewe ambapo kanisa limejengwa kiroho na imani yetu ktk yeye inasimamia hapo.

Ule ufunuo kupitia Petro saa ile ( peter confession), ule uthihirisho  na uthibitisho mkuu wa Yesu  Kristo pale kaisaria-filipi  alipokuwa amekaa  na mitume chini ya miti  ya miforsadi (mulberry), ndipo ulipo weka msingi na maana kuu ya huduma yake  duniani. 

Katika hatua zote za  maisha  ya Yesu  duniani,   wakati akisubiri  kufunuliwa   kwake  mioyoni  mwa  watu ile saa  iliyokusudiwa   na Mungu  baba, ukamilifu wake ulifikiwa kwa watu kumuelewa  yeye aliye mwana wa adamu kama mwana wa Mungu, na ilimchukua muda kueleweka hivyo sababu ufahamu wa binadamu unachelewa kuchanganya (slow to wit) inapokuja kuhusu  mambo ya rohoni, na hiyo ni kweli.

Yesu alipita stage ya utoto kama mwanadamu wa kawaida (conscious inakuwa dimly ktk kujitambua), then ya pili ya kujitambua,  roho anaanza kujifunua ndani yake ktk ujana na mpaka ukubwa wake (pale conscious iko light-up, anakuwa aware mambo mengi ya divinity na mission yake), ya tatu ni ubatizo, kujithihirisha kwa Mungu kwake  kama mwanae  na kuanza huduma  kama  mwalimu wa ufalme wa  Mungu, then mwalimu na mponyaji, hapa watu wa karibu walimjua kama mwana  wa  adamu na wengine wakamuita mesia, wengine  wakataka  hata  awe mfalme wa wayahudi, na  stage ya 4 na ya mwisho ilianzia  pale kaisaria-filipi alipofunuliwa  kama mwana wa Mungu na mpaka kusulubiwa kwake na kifo cha msalaba, na  ktk stage  zote hizo Yesu hakujikuza bali ulikuzwa  kwa namna alivyokuwa anaishi, its stages  kama ukuaji  wa kipepeo  kutoka buu, its  marked the new start  when  was observed change supernaturally organically.

Can you  be the son of God? Unaweza kuwa mwana wa  Mungu?

Yes! nasema unaweza kuwa mwana wa Mungu leo, kupitia  kumwamini kristo kama  Bwana  na  mwokozi wa maisha  yako.

Haya basi, nawe mwana wa Mungu  mwenye haki  kwa  roho wake mtakatifu kupitia ile imani ktk kristo   Yesu (Wagalatia 3:26), ktk kujitambua kwako hivyo pokea funguo za mamlaka  kuyatenda yaliyo makuu duniani kama  mbinguni, na huku sifa kuu ya umwana ya kuyatenda yaliyo mapenzi ya Mungu Baba, hata yawe magumu vipi iwe ni jadi yako, naye Mungu Baba akuwezeshe pale uyatendapo hayo mapenzi yake (Yohana 5:19; Luka 22:42-43) 🙏🏾.

Sunday, July 14, 2024

#PRAYER SECRET (SIRI YA SALA)


Sala/prayer imetokana na neno la kigiriki "proseuche" ikimaanisha- a wish, desire, request, or vow.  Hi ni kutokana mtu anamahitaji yake au shauku maishani mwake.

Sala ni package; kuna kukiri, shukurani, kusifu Mungu, kumtukuza na kumwabudu Mungu, kuomba msaada. Yaani ni zaidi ya dua.

Sala ni mawasiliano na Mungu ktk nafasi yako ya kimamlaka uliyopewa duniani.

“The ultimate object of prayer,” says The International Standard Bible Encyclopedia, “is not merely the good of the petitioner but the honor of God’s name.”

“Lengo kuu la sala,” yasema The International Standard Bible Encyclopedia, “si kutimiza faida ya mwombi tu bali heshima ya jina la Mungu."

Bill Graham ashawahi sema; "Prayer is not just asking, it is listening for God orders". ikiwa na maana Sala sio tu kuomba omba (kuna zaidi ya hilo), kuna kusikiliza matakwa ya Mungu pia.

Na kuomba sio tu kupiga kelele; kuna kuzungumza na Mungu kwa hoja zenye mashiko (Isaya 41:21), mfano wa Mfalme Hezekia (2 Wafalme 20:1-11), pia kuna kusali kwa siri (Mathayo 6:6).

Kuna mifano ya aina nyingi ya sala ktk biblia, umewahi kuwaza Cornelio alikuwa akisalije? (Matendo 10:2-4), ama kwanini Yesu alitolea mfano wa Sala za mtozaushuru na falsayo (Luka 18:10-14)?

Yamkini hatupati sawasawa na tunavyosali sababu pengine ni kule kusali vibaya kama mtu usiyejielewa (Yakobo 4:2-3), kwani sala ni mawasiliano na mbingu juu, kuna itifaki na taratibu kumfikia Mungu kwa unavyotaka kutendewa.

Na ni sharti umuendee Mungu ukijua ni mkuu kuliko matatizo yako, imani ya matarajio yapaswa iwe kubwa. Na pia toa na sadaka madhabahuni unaposali kama Cornelio, madhabahu inajengwa na sadaka zako, na hakuna madhabahu ikiwa hakuna sadaka, kwa maana hiyo madhabahu inaweza kuanzishwa sehemu yeyote ikiwa tu sadaka imehusika, kama Yakobo ili iwe madhabahu alipoota malaika wakipanda na kushuka alisali pale na kuweka ahadi ya kumtolea sadaka Mungu pale. Kumbuka Mungu aliona, anaona na yajayo ayaona na kujua yote. Hivyo ni kwa sadaka madhabahuni, Mungu anaona moyo wako na heshima unayompa, na Marko 11:17; anasema mahali pa madhababu ya Bwana ni nyumba ya sala, napo haikumaanisha ni kuomba tu, hapana, kuna zaidi ya hayo kama kuimarisha mahusiano na Mungu.

Siri ya maombi/sala zinazojibiwa ni pamoja na kujua nini usali na nini uombe  na ni wakati gani?, mahali gani? pa kusali na kuomba, na sio kusalisali na kuombaomba ilimradi unapayuka tu. Hapana, kuna sala zingine unazungumza na Mungu kwa utulivu kabisa na kisha utake kumsikia Mungu anasemaje juu ya ombi lako, zingine unaomba hili na lile huku ukidadavua kwa nini akupe wewe, zingine ni shukurani tu, zingine za hoja za msingi unakomaa na Mungu na reference kwa nini kung'ang'ania unachong'ang'ania kiwe. Zingine za kimamlaka unatiisha, unatangaza na kuamuru ziwe kutokana na mamlaka ya neno uliyopewa, na zingine ni mapambano, sala za vita ni kama kinywa kinatema risasi mfululizo kwenye ngome za maadui, watesi wako,  kukemea pepo na roho za kichawi na uganga.

Kwa mkristo sala na maombi ni silaha pekee, ya kumthibitisha yeye ni nani ktk mbingu ya Mungu na mamlaka gani yuko nayo kuitiisha dunia na kuamuru mambo yatokee kwa matakwa yake kama Bwana mwenyewe amupavyo kutenda🙏🏾.

Saturday, June 29, 2024

#PAY ATTENTION/ KUWA MAKINI


Sikio lina shepu kama vile tumbo la uzazi, ikiashiria chochote utachosikia kizuri ama kibaya, kitakuwazisha kama kusema kukutungisha mimba, na kupelekea kuzalisha kitu au jambo kama mimba/wazo lake kwa wakati na ule muda muafaka.

Hivyo kazi ya sikio ni kupelekea kuzalisha matokeo ya kile unachokisikia na kukisikia tena na tena, hakuna makosa hapo ni kutokeza matokeo. Na ndio maana hata biblia inasisitiza kuzalishwa imani kupitia kusikia neno la Mungu (Warumi 10:17). Na sasa kama imani huja kwa kusikia, nashangaa ni yepi mengine huja kwa kusikia? je' ni vipi kama hata unavyojisikia leo, vile unavyofeel vimepitia mlango huo huo wa sikio?

Na ndio maana tunasema PAY ATTENTION yaani KUWA MAKINI, sababu hata wakati wa Covid19, ni taarifa tulizosikia mara kwa mara ndizo zilitushitusha na kutupelekea kuwa na hofu kuu hata kuogopana na wengine kujificha. Hivyo hata ATTENTION ni kama currency ktk kizazi chetu, yaani ona ukisema pay attention, ni ya thamani, ni kama vile lipia pesa, attention ndio pesa yenyewe, sio rahisi ni gharama ni sacrifice, na hivyo ukipay attention utakipata na usipopay attention hutakipata, na pia attention ikipatikana inatransact na kunakuwa na exchange sababu inaweza onekana na kuhesabika, watu wanatransact agenda zao kupitia hiyo, mipango, kurubuni watu, kufunga na kufungua watu kifikra, kunadi vitu, Mungu na biashara na hata kuwaibia, na ni namna nyingi zinatumika kuipata attention kwa watu kwa mifumo yote ya mawasiliano. Na hii ni kweli kabisa nimeona ushawishi wa madalali, wapiga debe, watumishi wa Mungu feki na wa kweli, watu wa biashara ya mtandao, wa kwenye upatu, zama za babu wa roliondo, waganga, wanasiasa ile nguvu inayotumika kupata attention za watu ni kubwa naweza sema ni uwekezaji ni mtaji sababu ya tumaini la faida inayotokana na attention hizo.

Na ndio maana social dilemma documentary inasema "kama hulipii product, basi wewe ndio product, sisi ni products sokoni,  ule umakini wetu ndio product yenyewe inayouzwa kwa advertisers. Mitandao ya kijamii sio nyenzo/chombo; ni dawa tena ya kulevya." Attention za watu ndio dhahabu ya social media.

Yesu alisema kuwa mwangalifu/makini na unachokisikia (Marko 4:24). Kwa maana matamanio yetu hayatuamulii hatima zetu bali vile tulavyo. Yaani hiyo  ni vya rohoni na mwilini; iwe kwa masikio, macho, ndimi, ngozi, pua. Unajua unaweza kuwa na shauku ya kupunguza mwili na kuwa na afya njema, na hakuna kitakacho kusaidia kama unakula kula hovyo, ndivyo ilivyo na mambo ya rohoni pia. Hivyo chunguza na kuwa mwangalifu na unacholisha roho yako, unakuta vitu vya dunia vinakutawala, miziki ya kidunia inakushika, kuangalia picha za ngono, kuangalia filamu za kutisha na hata huogopi tena, kupenda sana zana za upako unazouziwa, hivyo angalia sana shauku ya nafsi kutamani vya dunia sana isikufunge usijekengeuka na ukajipoteza. So, be selective sio kila kitu cha kupay attention, usije corrupt nafsi yako, vingine ni kuvipuuzia ili kulinda nafsi yako.

Ona kwenye miji mikubwa; chokoraa/homeless wanapenda kuokota chakula kwenye matakataka ya nyumba za watu wengine. Kwa hiyo kama unataka kugeuzwa na kukuwa kifikra we uliyeamini, acha kuwa chokoraa kiroho, ungana kanisa karibu nawe ukuwe. Kula na tafakari (feed&chew) neno la Mungu na sio ya kidunia yaani toxic worldly content. Wafuate watumishi wa Mungu, walimu watakaokufunza kweli ya Mungu na kukuvuta katika utakatifu. Kumbuka njiwa hula vya kijani na kunguru penye miozo; cheki rangi ya muonekano wao, kuwa njiwa na sio kunguru.

Mwisho soma waraka wa Paulo kwa wafilipi 4:8, ubarikiwe na Bwana, amina.🙏🏾