#NIDHAMU YA BWANA, KWANGU MIMI NI NGUVU

Biblia takatifu inasema katika waebrania 12:5-11 ya kuwa;
Je, mmesahau yale maneno ya kutia moyo ambayo Mungu anawataja ninyi kuwa wanawe? "Mwanangu, usidharau adhabu ya Bwana, wala usife moyo anapokukanya.
Maana Bwana humwadhibu kila anayempenda, humpinga kila anayekubali kuwa mwanae."
Vumilieni adhabu kwani ni mafundisho; Mungu huwatendea ninyi kama wanawe. Maana ni mwana gani asiyeadhibiwa na baba yake? Lakini msipoadhibiwa kama wana wengine, basi, ninyi si wanawe, bali ni wana haramu. Zaidi ya hayo sisi tunawaheshimu wazazi wetu waliotuzaa hata wanapotuadhibu. Basi, tunapaswa kumtii zaidi Baba yetu wa kiroho ili tupate kuishi. Wazazi wetu hapa duniani walituadhibu kwa muda, kama wao wenyewe walivyoona kuwa vema; lakini Mungu anatuadhibu kwa ajili ya faida yetu wenyewe, tupate kuushiriki utakatifu wake. Kuadhibiwa si jambo la kufurahisha bali la kuhuzunisha. Lakini wale waliofunzwa kuwa na nidhamu mwishowe watavuna tuzo la amani kutoka katika maisha adili!.
Daudi pia katika Zaburi ya 23:4 anasema gongo lake na fimbo yake Bwana vyafariji.
Bwana Yesu niadhibu, nikanye na nipinge napokosea na kutenda visivyostahili kwa neno lako niwe mtoto mwema daima, kwa maana amri ni taa na sheria ni nuru, nayo makaripio ya nidhamu ndiyo njia ya uzima (Mithali 6:23), Amina.

No comments:

Post a Comment