#MUNGU HUTUMIA NGUVU ALIYOWEKA NDANI YA MWANADAMU NA MWANADAMU HUHITAJI NGUVU YA MUNGU KUTENDA JAMBO LOLOTE

      Mungu hutumia nguvu aliyoweka ndani ya mwanadamu, na Mwanadamu huhitaji nguvu ya Mungu kutenda jambo lolote liwe la Ufalme wa Mungu au sio, Hivyo Mungu hutenda kazi wakati wanadamu watendapo kazi (Waefeso 3:19)

Wakati Yesu alivyowaita mitume wawili, walikuwa sio wamekaa tu bali walikuwa wanatenda kazi,,,,,,,,,, Wavuvi……. Na Yesu akasema Njoo na unifuate mimi name nitakufanya mvuvi wa watu. Sasa ona….Mitume mwanzoni kabla ya utume hawakuwa wamekaa nyumbani tu pee! Kunywa chai na kahawa au kucheza bao sivyo. Luka 10:2 Yesu akasema; Mavuno ni mengi lakini watenda kazi ni wachache. Mungu anawatafuta watendakazi hodari walio watakatifu ambao wanaweza kudumu hata hali iweje iwe barafu iwe mvua ama kiangazi ama kipupwe yaani hali zote katika mwaka, Petro na Andrea walibadilisha kazi zao kwa kazi ya Bwana Yesu kristo kwa kuwa Kazi ya Yesu kristo ni bora zaidi yaani Kazi ya Ufalme wa Mungu. Unalipwa ujira na faida kila uitendavyo kazi yake kwa mfumo wa Baraka, kibali na mashitaka na ukifika mbinguni unavikwa taji……. 

Najisikia Kama kufanya kazi, Barikiwa na utende kazi Bwana Yesu wa Nazareti akukute kwenye kazi yako akutumie na kukubariki na kukupa kibali zaidi na zaidi.

No comments:

Post a Comment