#NGUVU YA MUNGU NDANI YAKO NA UFAHAMU NDIYO VITAKAVYOONGEZA MILIKI YAKO

     Kutoka 23: 29-30 inasema;”Sitawafukuza mbele yako katika mwaka mmoja; nchi isiwe ukiwa, na wanyama wa bara wakaongezeka kukusumbua. Nitawafukuza kidogo kidogo mbele yako hata utakapoongezeka wewe na kuirithi hiyo nchi.” Mistari hiyo ya Biblia inasema kidogo kidogo utamiliki mpaka utakapokuwa na uwezo wa kutosha yaani kule kuongezeka kwa kiwango sahihi cha kurithi na kumiliki vyote. Ni mpango wa Mungu tumiliki na kutawala vyote na siku zote akitaka kutupandisha juu anatuandaa kushinda vizingiti vilivyo mbele yetu ili kuweza kumiliki na kutawala kwa nguvu inayoachiliwa ndani yetu. Kwa sababu anajua pasipo maandalizi ya kutuwezesha sisi kwenda hatua nyingine twaweza athiriwa vibaya hatua hiyo mpya, Kwa hiyo unapata sawasawa na ulivyoandaliwa kupata, na ukishaandaliwa hakuna kitu cha kuzuia unachopaswa kukipata hata ije nguvu ya aina gani? Hata hivyo hakuna nguvu inayozidi jina la YESU wa Nazareti kwani nguvu zote ni za Mungu.

Ndio maana hata Daudi kabla hajainuliwa hadi kuwa Mfalme wa Israeli; aliuwa simba, dubu waliyetaka kula mifugo ya babaye ndipo akaja akamuuwa Goliath ambaye jeshi la israeli lote lilimuogopa ingawa alidharauliwa vivyo hivyo Samson, Musa, Gideoni. Kwa hivyo tunaandaliwa kuwa washindi! Lakini yapasa kumtumainia Mungu na kumwamini yeye tu!.

Galatia 4:1-2 inasema;” lakini nasema ya kuwa mrithi, wakati wote awapo mtoto, hana tofauti na mtumwa, ingawa ni bwana wa yote, bali yu chini ya mawakili na watunzaji hadi wakati uliokwisha kuamriwa na baba". Katika maisha huwezi kukabithiwa kila kitu kilicho urithi kwako mpaka ukue kiundani yaani kifikra, Kiakili, kimtizamo na uwe na fahamu wa kutosha la sivyo urithishwavyo vyaweza visiwe faida kwako kama ilivyokusudi na yamkini vikakudhuru. Siunajua hata baunsa wa kubeba uzito mkubwa hapimwi kwa ukubwa wa mwili au umri (yeye anajijua) bali nguvu ndani ya mwili wake iliyojengwa na misuli kakamavu, ndivyo ilivyo kwa hiyo, usikulupukie ukiona mtu yuko juu kuna gharama kwa njia moja au nyingine na pia ni neema ya Mungu, hata hivyo kuitunza nafasi au hatua uliyopo ni gharama pia, kwa hiyo tujifunze kuwaheshimu walio juu yetu tupate thawabu zao. Pia ondoa shaka na hofu Isaya 54:2-3 inatuamuru pasipo kufikirifikiri sana tutanue hema zetu (mipaka) kwa maana yeye Mungu ndiye atakayetuongeza kulia na kushoto sisi wenyewe hatuwezi kufanikisha jambo lolote lituhusulo pasipo msaada wa roho wake mtakatifu, hivyo tanua umiliki wako yawapi? maono yako kwa kiasi chochote kile Mungu ndiye jawabu katika Jina la Yesu wa Nazareti, Amina.

2 comments:

  1. Shalom mtumishi wa Mungu, SoMo lako ni zuri lakinimaadishi ni madogo sana

    ReplyDelete