#KWA YESU WA NAZARETI SISI NI WAKUU

       Kubaki ktk ukuu uleule, umuhimu uleule na ujasiri uleule na kuzidi ni kupitia Yesu kristo wa Nazareti tu; na ni kwa neema ya Mungu. Simama imara katika nafasi yako Mungu siku zote ni muaminifu hakika atakupandisha juu kila iitwapo leo kwa maana kuna kuongezeka Kiroho katika kristo kama mmea ulivyouona jana si uko hivyo leo, je si zaidi kwako mwanadamu uliyeumba kwa sura na mfano wake kule kuongezwa kwako. Unajua hata Mkuyu huanza kama Mboga lakini cha ajabu Mkuyu ukikuwa hauwezi kurudi tena kuwa kama mboga hata iweje majira yaje na yapite unazidi kuwa imara zaidi”. Hivyo nafasi uliopo kama ni Mungu amekuweka nawe ni mwaminifu kwake hata waombe vipi kurudi kwako chini wasahau. Biblia inazungumzia wa chini kwenda juu kwa wana wa Mungu (Kumbukumbu la Torati 28:13) na sio wa juu kushuka chini isipokuwa kwa shetani aliyeshushwa mpaka kuzimu (Ezekieli 28:13-19). Hivyo wa Juu hawezi kuwa wa chini bali huenda Juu zaidi ila wachini aweza kwenda Juu, ni kwa neema ya Mungu.

Biblia inasema katika Wafilipi 4:13; Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu na Zekaria 4:6; Inasema si kwa uweza wala si kwa nguvu bali ni kwa roho wa BWANA. Mwamini na kumtegemea Yesu wa Nazareti upate hatua mpya kila iitwapo leo, Amina.

No comments:

Post a Comment