#SISI SI WAJENZI WA MNARA WA BABELI BALI WAPANDISHAJI WA SALA ZETU KWA MUNGU ILI UTUKUFU WAKE UWE MKUU

      Kama vile ilivyokuwa kwa Kornelio; Jemedari wa Kikosi cha Italia katika Matendo 10:1-4, nasi tunapandisha na kupeleka sala zetu kuelekea juu sana pasipo kuchoka ambazo ni za kukumbukwa na kuwa manukato mbele ya Mungu; Ili ya kwamba kwa sala zetu hizo Mungu aweze kushuka kutuponya, kutuweka huru na kutubariki. Kwa maana katika hili hakuna mafarakano wala matengano kama ilivyotokea walipokuwa wanajenga mnara wa babeli ( Mwanzo 11:7-9) bali ni maelewano, kunia mamoja na kuwa na umoja katika kristo yaani mwili mmoja unaoshirikiana kwa sauti moja ya Roho mtakatifu kupitia sala zetu (Matendo 2:1-4). Kilichotokea wakati wa ujenzi wa mnara wa babeli, walikusudia kutenda hivyo ili wakamwone Mungu lakini kusudi lao halikuwa mpango wa Mungu naye akawasambaratisha kwa kuwachafulia usemi wasielewane yaani wasinie mamoja, lakini sasa tunalotumaini kupitia Yesu kristo aliyetuunganisha na Mungu kwa upya ambapo kwa sala zetu Mungu hushuka katika yetu kwa utukufu wa jina lake.  
        Hivyo ijapokuwa ndimi zaweza kutofautiana; yaani zile lugha tutumiazo katika kuwasiliana Roho Mtakatifu aliye mmoja ndiye atuwezeshaye sote kuwa wamoja. Ujasiri upo; sala zetu na ziwe kama mnara unaelekea juu sana kwa Mungu mwenyezi ili kupitia hizo Mungu atukuzwe na kushuka na kufanya makao ndani yetu kwa njia ya Roho mtakatifu, katika jina la Bwana na mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti, Amina.

No comments:

Post a Comment