#ROHO MTAKATIFU YU! KATIKA WANA, JE WEWE U MWANA WA MUNGU?

Roho mtakatifu huja kwa wana kama msaidizi ambapo kwa huyo tunalia, Baba! [Warumi 8:15]. Kwa hiyo kama Roho mtakatifu akikujia maana yake wewe ni mwana wa Mungu, na tunajua na kufahamu vizuri kabisa uhusiano kati ya Baba na Mwana upasavyo kuwa, kwa hivyo acha kuishi kama yatima, usiishi kama Mwanadamu aliyepokea roho ya kitumwa yaani roho inayomfanya kuwa mtumwa inayompelekea kuwa na hofu tena kama ya zamani pengine na kuzidi. Biblia katika Yohana 1:12 inaeleza ya kwamba kwa wale wote waliompokea YESU KRISTO wa Nazareti, aliwapa uwezo/Nguvu ya kufanyika kuwa Wana wa Mungu, na hata wale walioamini katika jina lake. Nguvu za Mungu zi ndani yenu, nyie mlio wana wa Mungu, na tulichopokea kutoka kwa mwenyezi Mungu hakika ni roho ya kutufanya kuwa watoto wa Mungu yaani Roho itupayo haki ya uwana.

Naam! Kuna faida zipi katika kuwa na Roho mtakatifu ndani yako;
“Akija yule Roho wa kweli atawaongoza muijue kweli yote. Yeye hatanena kwa uwezo wake mwenyewe bali atanena yote atakayosikia. Atawafundisha kuhusu mambo yote yajayo.  Atanitukuza mimi, kwa maana atayachukua yaliyo yangu na kuwaambia ninyi. Vyote alivyo navyo Baba ni vyangu, ndio maana nimesema kuwa atachukua yaliyo yangu na kuwaambia ninyi.” [Yohana 16:13-15]

Uwapo mwana wa Mungu, vyote alivyonavyo Mungu huwa na haki navyo, yaani huwapa wana wavitumie. Hii ni kwa sababu, u-wana kwa Mungu hukupa haki ya kufanyika mrithi pamoja na Kristo, kwa Mungu wetu. [Warumi 8:17].

Hii ni kweli; Roho mtakatifu yu ndani ya wana wa Mungu, je’ wewe ni mwana wa Mungu? Kumbuka wote walio katika Kristo YESU wa Nazareti wana kibali hiki katika yeye [Waebrania 1:5].

Mpokee Yesu Kristo wa Nazareti sasa!, kumpokea Roho mtakatifu na kuwa mwana wa Mungu hakika.


No comments:

Post a Comment