#WATATU WAKUTANA NA YESU WA NAZARETI

        Watu watatu wakutana na Yesu. Mmoja akutana naye karibu na mlima wa kalvari na mwingine akutana naye akiwa amesulubiwa msalabani na wa mwisho miguuni mwa msalaba alioangikwa Yesu.
Watu watatu wakutana naye wakiwa na asili tofauti mmoja ni mwafrika mkulima, mwingine ni mwizi na mwingine ni jemedari wa Roma. 
Watu watatu walikutana na yesu nao ni Simon mkrene aliyelazimishwa kumsaidia Yesu kubeba msalaba (Marko 15:21), Na mwingine mhalifu yule aliyesulubiwa pembeni ya Yesu (Luka 23:40-42) na mwingine ni jemedari wa Roma ambaye alikuwa hajali, hana utu, katili na muuaji (Luka 23:47).

Lakini wote walikutana na Yesu wakabadilishwa na kuwa viumbe vipya.

Bwana Yesu ninaposimama miguuni pako nikitazama msalabani kama ilivyokuwa kwa Simon, unitie nguvu niweze kubeba mizigo yangu, Na ninapomuona yule mhalifu na uliyomtendea, aibu zangu na dhambi zangu zikome, na ninaposimama na yule jemedari wa Roma nikuone mpya kila wakati. Univunjie mazoea yangu na kunigusa maisha yangu na tena nipate nguvu mpya za kiroho, kwani ukristo ni zaidi ya mazoea na ni zaidi ya yote yatendekayo ndani ya siku. Ni kumjua Yesu, nikuwa na moyo wa unyenyekevu mbele zake na kuwa na upendo wa kweli kwake kwa kufanya yampendezayo Mungu mwenyezi na kudumu katika kweli yake.

No comments:

Post a Comment