#SULUHU YA MAHITAJI AU MATATIZO YETU IPO NDANI YETU WALA HAITOKI MBALI NASI

         Mungu tupe uelewe ili isiwe kama maneno ya Daudi katika Zaburi ya 82:5-7.
Imani iwepo ndani yetu na kuamini kusikotikiswa katika JINA LA YESU KRISTO wa Nazareti, kwa maana neno lasema ya kwamba jaribu litupatalo ni lile lililo ndani ya uwezo wetu wala silakutuzidi, na ndio pimio haswa la Baraka zitakazokuja baada ya kulishinda.

Mama yake Yohana na mama yake Yesu wa Nazareti walikuwa ni ndugu; Yohana na Yesu wa Nazareti wanaweza kuwa walicheza pamoja wakati wakiwa watoto pengine hata Sunday skuli walikuwa wanaenda pamoja. Wajibu wa Yohana katika biblia ni kutengeneza njia ya Bwana Yesu wa Nazareti ambaye mwanzoni hakumjua ingawa walikuwa karibu. Na wakati ulipofika aliianza kazi yake kwa mwongozo wa roho mtakatifu ya kuindaa njia ya Bwana na hali akitazama tazama yupi Katika ya waisraeli ndio “Kristo”.

Katika Yohana 1:31-34; Yohana mwenyewe anashuhudia alivyofunuliwa kuhusu yupi ndio “Kristo” hakika. Yohana akasema;” Mimi mwenyewe sikumtambua (au kwa lugha rahisi mimi mwenyewe sikujua kama ndiye huyu), lakini sababu yakunifanya nibatize kwa maji (au sababu iliyonipelekea niwe mbatizaji) ili ya kwamba yeye afunuliwe kwa wana waisraeli”. Mistari wa 32 Yohana anashuhudia vile roho mtakatifu alivyomuelekeza kuhusu “Kristo” anasema; Naliona roho mtakatifu akishuka toka mbinguni kama hua na akakaa juu yake (Kristo). Mistari wa 33 anasema; “na mimi mwenyewe sikujua, lakini yeye aliyenituma nibatize kwa maji” aliniambia “Mtu Yule utakayemuona roho mtakatifu ameshuka toka mbinguni na kukaa juu yake ndiyo atakayebatiza kwa roho mtakatifu. Na mistari wa 34 anasema” nimeona na kushuhudia ya kwamba huyu ndiye mwana wa Mungu”

kwa hivyo Yohana mpaka alivyoanza kubatiza; katika wengi aliowabatiza Kristo alifunuliwa kwake katika yao ambaye ndiye Yesu wa Nazareti ndugu yake na sio mwingine mtu wa mbali au asiyemjua hapo mwanzo, hii inashangaza sana.

Pia katika kitabu cha Mwanzo baada ya Mungu kutambua upweke wa Adam… soma Mwanzo 2:21-23; Biblia inasema Bwana Mungu alifanya usingizi mzito Adam naye akalala; Kisha akachukua ubavu katika mbavu zake na kupaziba na nyama pale alipoutoa. Na kisha Mungu kupitia huo ubavu alioutoa kwa Adam akamfanyia Mwanamke Hawa na akamletea Adam. Kama Nabii Eubert anavyosema Adam alikuwa mpweke bustanini wakati Ubavu wake ulikuwa ndiyo suluhu ya tatizo yaani ndio mke ambaye angemuondolea upweke, Kweli inashangaza na kufurahisha sana.

Katika Mathayo 13:44; Neno linasema “Ufalme wa Mungu unafanana na hazina iliyofichwa shambani, ambayo mtu baada ya kuiona akaificha tena; na kwa furaha ya hiyo akaenda kuuza kila kitu alichonacho na kununua eneo lile la shamba. Hivyo popote penye suluhu ya tatizo au ambapo tatizo lako limetatulika hapo imani yako na iwe hapo kwa gharama yoyote ile kwa sababu ufalme wa Mungu ni zaidi ya vyote.

Tambua shamba ambapo yule mtu matatizo yake yalitatuliwa kwa kuiona na kuitambua ile hazina, sehemu ya shamba hilo alipoiona hazina palijulikana nayeye tu na palikuwa na muunganiko naye, sasa ni kwamba mwanzoni hakujua wala wengine wote waliomzunguka lakini baada ya kujua hata hawa wengine hawakumzuilia kuipata kwani ni yeye tu aliyejua. Kwa hiyo ni wewe tu ndiye unayeweza kujua suluhu ya kudumu katika matatizo yako ambayo wala haitoki mbali nawe na itakufanikisha wewe tu na wale wengine watakao amini kwako baadaye. Suluhu ya matatizo haiwezi kupatikana mbali nawe ipo karibu na katika uwezo wa kuona kwako. Ufalme wa Mungu upo karibu nawe na unakaa ndani yako ukishakumwamini kristo na kuupokea wokovu, Hakika utakuwa na ule Ufalme wa Mungu, Amina.

No comments:

Post a Comment