#IJUE SIKU YAKO ILETAYO AMANI KWAKO

       Ndugu ambaye bado hujaokoka nasema "ijue siku yako iletayo amani kwako na siku yenyewe ndio hii sasa!" Neno kutoka (Luka 19:41-44>, Yesu wa nazareti yu mbele yako sasa anasononeka kwa ajili yako na kukuhurumia akikuita kwa jina lako upate kumrejea Muumba wako upate pumziko la milele, kwa kuwa yeye ndiye njia, kweli na uzima mtu haendi kwa Baba isipokuwa kupitia kwake (Yohana 14:6). Naye anasema nawe sasa “laiti ungalijua saa ya kujiliwa kwako ukupasayo amani ungelijiweka tayari na kuikwepa dhoruba ya shida na matatizo isiyokoma kwako”. Pia katika Ufunuo 3:20 anasema; Tazama! Nasimama mlangoni (moyoni) nabisha hodi, mtu akisikia sauti yangu na kufungua mlango nitaingia kwake. Kama uko tayari; Sema niko tayari Bwana Yesu wa Nazareti karibu roho mtakatifu nifanye mimi kutambua saa hii unitembeleayo nipate amani ya roho na kutoka vifungoni kwenye taabu na shida nyingi. Hivyo ndugu uliyekusudia omba nami sala hii ya toba kwa wingi wa neema zako Mungu katika jina la Yesu kristo wa Nazareti upate kuokoka, tamka ifuatavyo;
Bwana Yesu wa Nazareti nakuja mbele zako, mimi ni mwenye dhambi nimeamini kuwa ulikufa msalabani kwa ajili yangu mimi, ninatubu dhambi zangu zote, Bwana Yesu nisamehe, Damu yako ya thamani iliyomwagika pale msalabani inioshe niwe huru na kunifanya mpya kabisa, futa jina langu kwenye kitabu cha hukumu, andika jina langu kwenye kitabu cha uzima, Roho mtakatifu niwezeshe kutenda mema katika dhamiri safi daima na milele, Katika Jina (YESU) la Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho mtakatifu, Amina.

Kiri maneno haya kwa ushindi kwamba nipo huru! nimezalia upya!, ya kale yamepita tazama yamekuwa mapya!, Asante Yesu wa Nazareti kwa kuniunganisha na Mungu baba, Asante kwa kufanyika njia, Kweli na uzima kwangu, Asante kwa roho mtakatifu, Amina.

No comments:

Post a Comment