#KUTENDA KAZI YA MUNGU NI KUMWAMINI ALIYETUMWA NA MUNGU

Ni kusudi la Mungu;
- kuunganisha dunia na mbingu pamoja kupitia mwanadamu, 
- kubariki kupitia mwanadamu, 
- kufundisha kupitia mwanadamu, 
- kuhukumu kupitia mwanadamu, 
- kutawala kupitia mwanadamu.

Yesu wa Nazareti ni Adam wa pili ambaye ni roho ihuishayo (1 Wakorintho 15:47), ndiye Bwana, ndiye Kristo na Mungu mwana kweli ambaye kupitia yeye tunaunganishwa na Mungu Baba na kupata uzima wa milele. Kwa kuwa jina alilokirimiwa lapita majina yote yaani “YESU” jina la Mungu Baba (Yohana 17:11-12).

Hivyo tujue Yesu wa Nazareti;
- Ni mwana wa Daudi
- Ni mwana wa Ibrahim
- Naye alikuwa mwanadamu hakika hali yuna uungu ndani
- Ni myahudi
- Na ni Mfalme

Ni mapenzi ya Mungu kuzungumza na wanadamu kupitia mwanadamu aliyemchagua mwenye roho ahuishaye “Roho mtakatifu”. Baada ya Yesu wa nazareti (Adam wa pili) kupaa kwenda mbinguni, kwa neema za Mungu, watumishi wengi wa Mungu aliye juu kupitia Roho mtakatifu wamefanyika kiungo kati ya Mungu na wanadamu na Mungu awafunulia mengi kuhusu wanadamu wenzao na kuwafanya kuwa Baraka kwa wengine. Hivyo kazi ya Mungu haitatendeka ndani yako isipokuwa kwa kuwaamini waliotumwa naye. Katika Yohana 17:20 Yesu wa Nazareti anasema; “Wala si hao tu ninaowaombea lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao (ushuhuda wao kuhusu Yesu wa Nazareti)”. Biblia Katika Yohana 5:38 inasema; "na ujumbe wake (Neno) haukai ndani yenu maana hamkumwamini yule aliyemtuma". Yohana 6:28-29 inasema baada ya Yesu wa nazareti kuulizwa; ”Basi tufanyeje ili tupate kuzitenda kazi za Mungu? Yesu akajibu akawaambia, Hii ndiyo kazi ya Mungu, MMWAMINI YEYE ALIYETUMWA NA YEYE”, kwa hiyo kwa kuwaamini watumishi wa Mungu kuna kutenda kazi ya Mungu na kuliishi Neno.

Hakuna aliyekua pasipo kujifunza kupitia waliomtangulia kwa maana tukionacho twajifunza na tujifunzacho twakitendea kazi na kujaribu na kile tukitendeacho kazi na kujaribia ndio inakuwa kwetu hivyo yaani ndio utakavyokuwa na vile utakavyokuwa kuna matokeo mema. Kwa hiyo katika kumwamini mtumishi wa Mungu aliyetumwa na Mungu kuna mafunzo kuhusu Mungu aliyemtuma na zile kazi za Mungu azitendazo, nawe utazitenda na zaidi ya hizo kwa maana hakuna mwanadamu aliyemuona Mungu wakati wowote ule isipokuwa Yesu kristo wa Nazareti (Yohana 1:18; Kutoka 33:20). Sema namwamini Mtumishi wa Mungu ninayesimama chini yake ya kuwa ni Mungu ndiye anazungumza ndani yake, matokeo yake ni Baraka, hatua mpya, ulinzi, hekima na mengineyo kama ulivyo uhitaji wako, Amina.

No comments:

Post a Comment