Biblia inatuasa sana kuikimbie zinaa, na ya kwamba kamwe usiruhusu
moyoni wako kushikwa katika tamaa itakayo kupelekea kuzini na kisha kupoteza nafsi yako iliyo ya thamani.
Maonyo ya Biblia juu ya zinaa;
[1 Wakorintho 6:18-19]
"Ikimbieni zinaa. Kila
dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa
hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe. Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni
hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si
mali yenu wenyewe".
[Mithali 6: 25-29]
"Usiutamani uzuri wake
moyoni mwako; Wala usikubali akunase kwa kope za macho yake.
Maana kwa malaya mtu
hutiwa katika hali ya kuhitaji kipande cha mkate; Na kahaba humwinda mtu anase
nafsi yake iliyo ya thamani.
Je! Mtu aweza
kuua moto kifuani pake, Na nguo zake zisiteketezwe?
Je! Mtu aweza
kukanyaga makaa ya moto, Na nyayo zake zisiungue?
Ndivyo alivyo aingiaye
kwa mke wa jirani yake; Kila mtu amgusaye huyo atakuwa na hatia."
[ Mithali 31:3]
"Usiwape wanawake nguvu
zako; Wala moyo wako usiwape wale wawaharibuo wafalme."
[Mithali 6: 32-33]
"Mtu aziniye na
mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake. Atapata jeraha na
kuvunjiwa heshima; Wala fedheha yake haitafutika."
Amina.
No comments:
Post a Comment