#SADAKA YAKO IWE KAMILI SIKU ZOTE FANYA KAMA KWA BWANA

Peleka zaka kamili gharani kwa Bwana ili ubarikiwe………Malaki 3:10.
Mwanzo 22:7; Na Isaka (ambaye ni sadaka) akamuulize Ibrahim babaye, akasema Baba yangu, Ibrahim akasema nipo hapa mwanangu, na ndipo alipomwambia tazama! Moto upo na kuni zipo, lakini yuko wapi mwanakondoo wa sadaka ya kuteketezwa? Sadaka au Matoleo yanatakiwa yawe ya kukugusa na sio tu ili mradi sadaka. Lakini inapotokea sadaka kumuuliza mtoaji kuwa tunakila kitu katika tendo la utoaji lakini SADAKA IKO WAPI?, ina maanisha kuna shida hapo na kwamba sadaka inajua kuna sadaka inayostahili sio tu yenyewe kama ilivyo. Ukisoma Luka 21:1-4 inasema "Yesu akainua macho yake akawaona matajiri wakitia sadaka zao katika sanduku la hazina. Akamwona mjane mmoja maskini akitia mle senti mbili. Akasema, Hakika nawaambia, huyu mjane maskini ametia zaidi kuliko wote; maana, hao wote walitia sadakani katika mali iliyowazidi, bali huyu katika umaskini wake ametia vyote alivyokuwa navyo". Malaki 1:6-9 inatuonya juu ya utoaji wa sadaka ambazo ni vilema, ambazo hata ukimpa mwanadamu mwenzako haimbariki sasa je’ si zaidi kwa Mungu wa Mbinguni?

Bwana Yesu wa Nazareti tuwezeshe ili tuweze kutoa sadaka kwa moyo wa imani inayogusa, malimbuko na matoleo mengine na fungu la kumi ambavyo vinagusa mioyo yetu kabla hata kugusa moyo wa Mungu na wale tunaowatolea iwe maskini, mjane, yatima, watoto wa mitaani au kuitegemeza huduma ya kristo na wengine wenye uhitaji, kwani tunaamini katika njia hiyo baraka ni nyingi. Hivyo barikiwa na sadaka yako kabla haijabariki wengine la sivyo ni kazi bure mbele za Mwenyezi Mungu, Amina.

No comments:

Post a Comment