Ukikua kiroho, mwili wako hautaweza kufanya chochote pasipo kuthibitishwa na roho wa Mungu ndani yako. Na hapo ndipo uwezapo kushinda matamanio ya mwili na dhambi. Kiwango chako cha nguvu katika roho kinatambuliwa na namna wewe uwezavyo kuushinda mwili na kumtii Mungu. Biblia 1 Yohana 5:4 inasema“Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu.” Twasisitizwa juu ya imani katika kristo ya kuwa ndiko ushindi ulipo na ya kwamba pasipo imani ni ngumu kumpendeza Mungu (Waebrania 11:5-6). Kwa maana amwendeaye Mungu anapaswa kumwamini yeye yupo na kwamba huwapa dhawabu wale wamtafutao, hivyo kuushinda ulimwengu ni ile imani yetu na ndiyo itakayotuelekeza kupitia roho mtakatifu na kutupa signal yale tupaswayo kuyatenda yaliyo ya haki na yale tusiyopaswa.
Aliye na Imani katika Mungu ni yule aliyezaliwa na Mungu kwa namna ya Roho mtakatifu hivyo atamsikia na kumtii Mungu na hakika malango ya kuzimu hayatamshinda kutokana na ile imani. Jiendeleze wewe mwenyewe kiroho kwa kusoma Neno la Mungu. Warumi 8:5-9;Utakuwa mshindi wala dhambi haitakushinda kama ukidumu katika Neno, Toba, Kujitakasa, Shukrani, Sifa na Maombi. Amina

No comments:
Post a Comment