#WOKOVU ULIOTHIBITIKA KATIKA HAKI UNAKUFANYA KUWA RAIA HALALI WA UFALME WA MBINGUNI

Wokovu ni pasipoti inayotufanya kuwa raia wa ufalme wa mbinguni,
Wokovu ni cheti cha uraia wa mbinguni na nchi ile mpya ijayo, na wokovu ni kwa neema ila unathibitika katika haki ambayo i katika matendo mema tuyatendayo zile dhamiri zetu kuwa safi (chumvi safi). Kaa ukijua ya kuwa pia Mwanadamu kama Mwanadamu kamwe hawezi kuwa mtii wala mnyenyekevu mbele za Mungu na pia hawezi kuwa mchaji wa Mungu pasipo neema ya wokovu katika maisha aishiyo, la sivyo ni ubatili tu kwani tunafanyika raia na twaishi kama raia wa ufalme wa Mungu kwa Nguvu inayotuwezesha kuwa hivyo wala usidanganyike kwamba unaweza kwa kujinyenyekeza tu pekee au kujifanyisha mtakatifu ni ngumu sana papsipo Neema ya Mungu (Yohana 1:12).
Sisi si wa ulimwengu huu (Yohana 17:14) Yesu wa Nazareti anasema;”Nimewapa Neno lako nao ulimwengu umewachukia kwa kuwa wao si wa ulimwengu kama mimi nisivyo wa ulimwengu huu.”Na pia katika Yohana 17:16 Yesu wa Nazareti anasema“Wao si wa ulimwengu kama mimi nisivyo wa ulimwengu.”
Na ndio maana katika (Mathayo 17:24-27); Inazungumzia Swala la Yesu wa Nazareti kulipa kodi kwa maana sio raia, ndipo Yesu akamuuliza waonaje Simoni? Wafalme wa dunia hupokea kodi ama ushuru kwa watu gani? Kwa wana wao au kwa wageni? Petro akajibu kwa wageni ndipo Yesu akasema kwa hiyo wana wao huwaacha huru pasipo kulipa?, Yesu wa Nazareti akasema ili tusiwakwaze akamtaka Petro akavue kwa ndoano samaki na yule wa kwanza kuvuliwa afumbue mdomo wake atoe shekeli na akalipe kwa ajili yake na Yesu kwa kuwa si wa ulimwengu huu. Hivyo baada ya wokovu, kuishi kwako duniani ni kama kwa mtu wa kuja asiyetakiwa (chumvi), kwa maana kupingwa kwake ni kutokana na kuwa kuja kwa kweli huleta hukumu hivyo wengi wapinga kwa sababu kwa kweli ya Mungu unawahukumu lakini siku zote penye kweli Mungu yupo na atakupigania ndio maana hata Yesu wa Nazareti pamoja na kumpinga kwote lakini hawakuweza kumzuia kuinena kweli mpaka wakati ulioamriwa na Mungu.
Siku zote asiye raia hupingwa na raia labda ampendezeshe au amlembe yaani afanye vile raia wapendavyo (awe chumvi iliyoharibika), Ujio wa Yesu wa Nazareti ulipingwa hata kabla ya kuzaliwa kwake kutokana na kuwa Mungu alikuja duniani kuhukumu wenye dhambi kwa kuifunua kweli yake na yeyote aiaminiye anapata uzima wa milele lakini kwa asiyeamini hukumu.Hata kama shetani (Mshitaki wa Ndugu, Mr. Lawama, Mr. Kushindwa) alikuwa anataka kumuelezea Mungu kuwa sheria na amri zake ni ngumu kuzitimiza na kuzitenda ili awe na haki katika kuasi kwake lakini sasa kwa kuja Yesu wa Nazareti; Mungu kuishi kama mwanadamu katika aina yote ya maisha Shetani amekwishahukumiwa kwani Yesu wa Nazareti (Adam wa pili) alithibitisha kuwa amri na sheria za Mungu zaweza kutimizika na kutendwa kwa namna ya Roho Mtakatifu kule yeye kufanyika mfano kama mwanadamu. Shetani hata kabla ya kuzaliwa kwa Yesu wa Nazareti alijua kuwa huyo anakuja kutangua mashitaka yake mbele za Mungu apate hukumu na ndio maana anaharibu wanadamu wengi kwa kuwafanya watumwa wa dhambi zake ili asionekane kuwa ni yeye tu aliyeshindwa kutii na kutenda amri na sheria za Mungu. Ukisoma Biblia inaonyesha kuwa kuzaliwa kwake ilikuwa muujiza kwani watoto wote wa kiume pamoja naye, ilitolea amri na Mfalme Herode kuwa wauwawe huku tajeti ikiwa ni Yesu wa Nazareti ndipo malaika wa Mungu akamwambia Yusufu kuwa mtoto apelekwe Misri mpaka Mfalme Herode akifa ndipo aletwe (Mathayo 2:7-23). Ujio wa Musa pia ulipingwa na Farao wa Misri kwani waisraeli wote walikuwa kwenye kongwa zake yaani watumwa wake hivyo kwa kuwa Musa alikuja kama mkombozi wa waisraeli kuwapeleka nchi ya ahadi (kama sisi tulivyoahidiwa Yerusalemu mpya) Farao aliwataka watoto wote wa kiisraeli wauawe huku tajeti ikiwa ni Musa lakini Mungu alimponya kwenye kisafina (Kutoka 1:15-16 na 2:1-10) akaja kuwa mkombozi wa waisraeli. Hivyo Mungu akiwa upande wako utapingwa kwa kuwa sio raia wa dunia lakini hutashindwa utavuka tu kwani wewe ni kusudi kwa Mungu lakini kama Biblia itusisitizavyo kuwa tushike sana tulivyonavyo asije mwovu akatunyang’anya mataji yetu (Ufunuo 3:11). Pia tunamsoma Yusufu alikuwa akiishi vizuri na ndugu na familia yake kwa ujumla lakini siku tu Mungu alivyokuwa upande wake na kumfunulia mambo makubwa na kumfanya mkuu (raia wa ufalme wa mbinguni) ndugu zake na familia yote wakamchukia (Mwanzo 37:15-28) badala ya kumfanya msaada wao lakini pamoja na chuki zao baadaye wakaja kuinama mbele zake kama mkuu wao na kuupata msaada wake. Hivyo yote utendewayo Mungu akiwa upande wako yatakuja kudhihirika hapa hapa duniani na itajulikana kuwa Mungu hakuwa kwa watesi wako bali upande wake na Neno lake Mungu juu yako litathibitika na watesi wako watahitaji uwasaidie. Na kwa kuwa wewe sio raia wa dunia hata maongezi yako, ushauri wako, hekima zako, busara zako kwao wasioamini huonekana kuwa vita kwa ajili ya ile kweli ya Mungu na ndimi zao kufarakanishwa kama Yesu wa Nazareti alivyosema unadhani nimekuja kuleta amani duniani, la hasha! Bali moto, upanga na mafarakano kwa maana ndugu watafarakana kwa ajili ya kweli baba na mwana hwataelewana (Mathayo 10:34, Luka 12:49 na Luka 12:51). Tunasoma pia (1 Wafalme 22:13-38) kwa habari ya Nabii Mikaya na Mfalme Ahabu alisimama katika kweli ya Mungu kinyume na manabii 400 wa mfalme Neno lake Mikaya Nabii lililokweli ndio lililosimama mpaka mwisho pamoja na shida na taabu zote alizopata, Pia (1 Wafalme 17:1 mpaka 2 wafalme 2:11) kwa habari ya Nabii Eliya na Mfalme Ahabu na Yezebeli mkewe alisimama katika kweli ufalme ukampinga na wala hakupendwa nao lakini mpaka mwisho kwa kuwa alikuwa raia wa mbinguni na anayo ile pasipoti alitwaliwa na Mungu, Pia Nabii Isaya shida na taabu alizopata ni kutokana na kweli aliyoibeba ilihukumu watawala wa dunia hawakumfurahia wakamuuwa kinyama. Naye Samsoni Mnadhiri wa Mungu kwa kupenda kwake haki alisimama mwenyewe katika Israeli Mungu akawa pamoja naye na wafilisti walimchukia na kutafuta kummuua kwa kuwa waliwafanya waisraeli watumwa wao (Waamuzi 15:11). Katika Yohana 17:9 Yesu wa Nazareti anasema;”Mimi nawaombea hao, siuombei ulimwengu bali hao ulionipa kwa kuwa hao ni wako”, tunafanywa raia wa mbinguni kwa kuwa wana wa Mungu, ulimwengu unatuchukia kwa kuwa Bwana Mungu kwa neema ametuchagua na anatuombea tuponywe na dhiki ya ulimwenguni. Hivyo hatupendwi wala kufurahiwa kwa sababu sisi ni raia wa ufalme wa mbinguni na wala si walimwengu, ukichukia uovu (shetani), uovu utakuchukia kwa sababu dunia ndiko kuliko kitovu cha uovu kwa kuwa mkuu wa dunia hii aliyekwisha hukumiwa ni mwanzo wa huo. Dunia hii imeshachakachuka haihitajiki mbele za Mungu (lakini ipo neema ya Mungu kwa waaminio hupata wokovu na kuponywa na dunia) na ndio maana siku ya mwisho dunia hii itaondolewa yote na kutupwa motoni na wote waipendayo na vyote viijazavyo na kisha zitafanywa mbingu mpya na nchi mpya halafu itakuja Yerusalemu mpya ule mji wa Bwana wa wateule wake wote (Ufunuo 21:1-7). Lakini kaa ukijua siku zote masihi wa Mungu haguswi Mungu akiwa upande wake, Tunamsoma Danieli pia Meshaki, Shedraki na Abedinego, Danieli alisimamia kweli mpaka mwisho Mfalme Nebukadineza akaamini na kumtii na kukiri kuwa hakuna Mungu kama amwabuduye Danieli, watawala chini yake wakafarakana na Danieli kwa ajili ya ukuu ndani yake lakini mwisho alishinda(Danieli 6:3-24). Danieli walimuita Beltashaza katika ufalme wao,jina hilo hakushikamana nalo na halikuzoeleka isipokuwa Meshaki(aliyeitwa awali Mishaeli), Shedraki(aliyeitwa awali Hanania) na Abednego (aliyeitwa awali Azaria) majina hayo yalishikamana na huo ufalme (Daniel 1:6-7) na ndio maana hata sanamu ya mfalme ilipotegenezwa (Danieli 3:1-27) Meshaki, Shedraki na Abedinego ndio walilazimishwa kuiabudu na siyo Danieli, kwa hiyo pia kataa vyote visivyotokana na Mungu vilivyo vya dunia ili dhambi zao zisishikamane nawe wakapata kukutia hatiani. Amina