#WEWE NI MUIGIZAJI MKUU KATIKA SINEMA YA MAISHA YAKO

    Siku zote katika sinema/filamu muigizaji mkuu huwa hafi kwa sababu kama akifa haitakuwa na mvuto kwa watazamaji na wala hakutaweza kuwa na sehemu ya pili, ya tatu au ya nne ya filamu hiyo. Na kama ukiwa unaangalia sinema ya vitendo utaona kuwa wakati muigizaji mkuu au sterling anataka kama kuuawa vile lakini cha ajabu utakuta anapona na kuwa hai tena. Wewe ni muigizaji mkuu kataika sinema ya Mungu ambayo Yesu wa Nazareti ndio muongozaji mkuu na unajulikana kuwa wewe ni mshindi kivyovyote vile kuna sehemu unaweza kuanguka na kwa neema yake unasimama tena ukiwa na nguvu na imara zaidi. Unayoyapitia sasa ni sehemu tu ya kwanza unaweza ukaona kama unabanwa sana lakini utapona na kuvuka ikiwa kuna sehemu ya pili ya sinema inayokusubiri kuicheza na ya tatu na ya nne zote zinakusubiri mpaka sinema yote nzima ikikuonesha wewe ni mshindi mwishoni kama muigizaji mkuu. Usiogope wala usiwe na wasiwasi hautashindwa wewe ni muigizaji mkuu wanaweza kuonekana kama wanakushinda sasa lakini mpaka mwisho wa sinema wewe utahitimisha sinema hiyo kwa ushindi mkuu (shepherd Bushiri Nabii).

  Rejea katika biblia wafalme wa pili 7:3-10; Ilikuwa kama movie kabisa ambapo waigizaji wakuu walikuwa wenye ukoma wane na ilianza baada ya tamko kutoka kwa Elisha Nabii wa Mungu. Na movie ilianza mstari wa tatu ukisema; Na kulikuwa na wenye ukoma watatu katika maingilio ya geti. Mistari wa sita; kwa maana Bwana alikuwa amewasikilizisha Washami kishindo cha miendo ya magari, na kishindo cha farasi, kama kishindo cha jeshi kubwa; wakaambiana, Tazama mfalme wa Israeli amewaajiri wafalme wa wahiti, na wafalme wa wamisri, waje wapigane nasi 7; kwa hiyo wakaondoka, wakakimbia kungali giza bado, wakaziacha hema zao, na farasi zao, na punda zao na kimo chao vile vile kama kilivyokuwa, wakakimbia wapate kujiponya nafsi zao. Naupenda ule mstari wa sita kwa maana wale wenye ukoma walivyokuwa wanatembea BWANA akawasikizisha washami vishindo vya miguu yao wenye ukoma kama vile vishindo vya jeshi kubwa maana malaika walionyesha utisho kupitia hatua za wenye ukoma, nao wakaingia hofu na kukimbia kila mmoja upande wake waweze kuponya nafsi zao. Na hiki ni kipande cha muvi cha kushangaza ambacho yesu kristo amekiongoza ndani ya kitabu cha Wafalme wa pili 7. Hivyo ndugu usiogope wewe ni muigizaji mkuu katika sinema inayoongozwa na Yesu kristo na siku zote stering hauawi la sivyo hiyo sio sinema. Amina

No comments:

Post a Comment