#NENO NI MUNGU

BIBLIA ni Agano, Ahadi, Usia wa Mungu kwa wanadamu, lakini siri kubwa ni kuwa Neno ndani ya Biblia ni zaidi ya maandishi ni pumzi ya Mungu, ni uungu wa Mungu; NENO ni Mungu. Biblia inasema hapo mwanzo kulikuwapo Neno naye Neno alikuwapo kwa Mungu naye Neno alikuwa ni Mungu [Yohana 1:1], na pia Biblia inasema hapo mwanzo dunia ilikuwa utupu naye Roho alikuwa juu ya vilindi vya maji  akisubiri Neno apate kulitekeleza [Mwanzo 1:2]. Na Yohana mtakatifu anatuhakikishia kwa habari ya Yesu wa Nazareti kwamba lile lililokuwepo toka mwanzo, walilolisikia na kuliona kwa macho yao na kulitazama na mikono yao ikalipapasa ndio NENO la Uzima. Isaya 9:6 anatabiri kwa habari ya ujio wa Yesu wa Nazareti (Mungu mwana) duniani ambaye ni Neno la Mungu ya kuwa ni Mfalme wa Amani, Mungu mwenye nguvu na Baba wa milele.  Hata pale Tomaso mtume wa Yesu wa Nazareti alipomuomba awaonyesha Baba wa Mbinguni kuwathihirishia ili na wao wawe na uhakika zaidi pasipo shaka, lakini Yesu ajibuje kwa swala hilo, akamwambia Tomaso umekuwa nami siku zote hizi bado unasema nikuonyeshe Baba.
Hakika Neno ni Mungu, Gedioni aliyekuwa kijana akiwa hana hata habari ya kuwa mtu mkubwa, lakini Mungu akamtokea kupitia malaika wake na kumwambia “Gedioni ee! Shujaa”, cha ajabu kwa Neno hilo ambalo ni Mungu; Gedioni akawa shujaa mara [Waamuzi 6:11-12], hivyo Neno ni Mungu na ni nafsi ya pili ya Mungu na ni Mungu hakika.
Neno pia ni mzigo; ambalo ni kama ujumbe mzito ambao unapaswa kufikishwa sehemu husika kwa wakati ulioamriwa [Malaki 1:1], kumbuka habari ya Yona nabii alipojaribu kukimbia na uponyaji wa Ninawi, kwa sababu ni mzigo wa walengwa wengi aliokuwa amebeba akasababisha hata meli kutaka kuzama, kwa kuwa ni watu wengi aliowabebea uponyaji na Hatma ya maisha yao ilikuwa juu yake, kwa hivyo ya kwake yote aliyopanga hayakuwezekana bali kutimiza tu yale yaliyokuwa ya Bwana, (ndugu ukiwa na agizo la Bwana usitulie kwa kuwa ni mzigo utakaokukula mpaka ukatende sawasawa na agizo hilo). Ukisoma kwa habari ya Semioni na Anna nabii mke ule mzigo waliokuwa nao wa kusali kwa habari ya mkombozi wa dunia yaani Yesu wa Nazareti na sala zao zilimusukuma hata malaika Gabrieli kwa wakati ulioamriwa na Mungu kuwatokea kuhani Zakaria na Bikira Maria kama uthihirisho wa sala zao juu ya kuzaliwa mkombozi.
Zaburi 82:5-7; inatusistizia ya kuwa sisi ni miungu na wana wa Mungu aliye juu sana, hivyo tunapaswa kujitambua kuwa uungu u ndani yetu pale Neno la Mungu ambalo ni Mungu liwapo sehemu ya maisha yetu. Tunapaswa kujitambua hakika, kwa maana mrithi awapo kama mtoto hana tofauti na mtumwa ingawa ni Bwana wa vyote [Galatia 4:1]. Jitambue na tambua Nguvu iliyomo ndani ya NENO ambalo ni Mungu tunasoma pia habari ya Mama Msamaria alipoonana na Yesu wa Nazareti ambaye ni Kisima cha maji ya uzima (Yesu) akiwa amekaa juu ya kisima cha Yakobo kirefu, bado mama Msamaria alikuwa akihangaika kutaka maji ya mbali na yasiyokata kiu hali maji ya uzima yalikuwa karibu yake na akizungumza naye.  jifunze kitu hapo kwanini wanadamu hutanguliza dharau mbele hata pasipo kujua kwa kina uwezo ulio ndani ya wanadamu kwa sababu unatofautiana sana, na ni heshima pekee ndio hufanya uweza ndani ya Mwanadamu kuwa na faida kwa Mwanadamu mwenzake. Huyu Mama Msamaria alimchukulia Yesu wa Nazareti kama Myahudi tu wa kawaida na kumbe alibeba uponyaji wake na suluhu ya maisha yake ilikuwa juu yake kwani yeye ni Mungu, ona huyu Mama alimwita Yesu “we Myahudi”, lakini dhidi Yesu alivyokuwa akifunuliwa kwake huyu Mama akaanza kubadilika katika viwango vya heshima alivyokuwa akimuchukulia, unaona Yesu wa Nazareti alivyoongea nae kwa kina yule Mama akamwita “Bwana”, jinsi alivyozidi kufunguka akamwita tena “Bwana”, kisha baadae akamwita “Nabii” na alipofikia kumwita na kumtambua kwamba ni “Kristo”, na NENO ndani yake ni Mungu kabisa, historia yake yote ikageuka na kufanyika mpya kabisa na saa ile ile yule Mama Msamaria akageuka na kuwa “Mwinjilisti na Nguvu sana” [Yohana 4:7-26].
Kijana wa Bwana jitambue sasa kwani kwake hakuna uzee, kama vile Maombolezo 3:27-28 inavyosema ya kuwa ni vema Mwanadamu aichukue nira wakati wa ujana wake hali ana Nguvu na akae pekee yake na kunyamaza kimya huku akiitazama njia yake tangu awali kwa sababu ni Bwana ameweka hayo juu yake. Kijana unapaswa kuielekea njia ya Bwana shetani anajua kwamba wnadamu hawana lolote na yoyote wanayoyafanya ni kwa ajili ya miili yao na maisha haya ya duniani pekee na wala hawajui chochote kuhusu baada ya hapa na ndio maana katika Ayubu 2:4 Shetani anasema 'Ngozi kwa Ngozi' kama vile wanadamu mwisho wa kufikilia kwetu ni kuhusu vinavyoonekana sasa na wala hatuna habari na vile tulivyoandalia rohoni, kwa maana hata Warumi 7 pia inatufahamisha kuwa miili yetu ni ya mauti na wala haiwezi kumtii Mungu.

Mwambie shetani najitambua na kwamba nitayaishi yale yamupendezayo Mungu kwa maana ndio Uzima wa milele na NENO ndaliishi hilo ili niwe na Amani, huru na kweli ikae ndani yangu daima kwani ndiye Mungu wala kuhukumiwa nafsi kusiwepo moyoni mwangu, mwili wangu kwa uweza wa Roho mtakatifu katika jina la Yesu Kristo wa Nazareti hautakuwa na uwezo tena wa kunivuta kwenye dhambi pasipo dhamiri yangu kupenda hivyo na siku zote nitatenda mema, ee’ Mungu nisaidie niwe huru milele, Amina.

No comments:

Post a Comment