Hakuna ugumu wala kanuni maalum
au kamili kuhusu utabiri wa ndoto. Naamini ni suala la ufahamu ingawa kuna
nyingine zinachanganya kiasi kwamba utahitaji kuutafuta uso wa Mungu kwa ajili
ya ufafanuzi wa ndoto hizo [Evang. Kenneth Onyene]. Kuna ndoto zingine si za
kawaida bali/ila ni Ufunuo/maono [yaliyofungwa]; na kama ambavyo Mungu anatumia
njia ya ndoto kuongea na sisi, tukumbuke hata shetani anatumia ndoto pia.
Hekima, maarifa yatokanayo na neno la Mungu ndiyo yatujuzayo kuwa ni maono ya
Mungu ama shetani. Ila tujue ndoto ni unabii binafsi, ni maono yaliyofungwa
[closed vision]. Kumb. 29:29; inasema kwamba "mambo ya siri, ni ya
Mungu wetu lakini mambo yaliyofunuliwa ni yetu sisi". Mungu hawezi
kukupa ndoto bila sababu ya msingi lakini hukupa ndoto kulingana na kusudi la
kuumbwa kwako duniani. Mungu alimuumba Yusufu- mwana wa Yakobo ili awe kiongozi
na alimpa ndoto Mwanzo 37:5-9. Mungu atakupa ndoto kukuonyesha vipaji vyako ili
kukuwezesha kuvitendea kazi kama Yusufu, Mungu pia hukupa ndoto ili kukuongeza
katika shughuli zako za kila siku kama Farao.
Inawezekana kabisa ndoto zako zote zikawa kama runinga unayoangalia moja
kwa moja. Lakini tukumbuke sio kila ukiota unamhitaji mtafsiri wa kutafsiri
ndoto yako, unachohitaji ni kusogea kwa Mungu kwa sala mpaka ufunuliwe maana
yake, kwani ni yeye aliyesababisha na kama si yeye pia utapata jibu tu. Kwa
maana ndoto ni unabii binafsi ambao Mungu hukupa ili kukuwezesha kuyajua mambo
ya baadaye. [Israel John O].
Tukumbuke pia Ayubu
33:14-16 inasema, “kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili,
ajapokuwa mtu hajali. Katika
ndoto, katika maono ya usiku, usingizi mzito uwajiliapo watu, katika
usingizi kitandani. Ndipo
huyafunua masikio ya watu, nakuyatia muhuri mafundisho yao.”
SALA:
Mungu Baba niwezeshe nami kuota na kuzitambua ndoto niziotazo na mafunuo yake yote ili niweze kuishi katika mpango na kusudi la Mungu katika jina la Yesu Kristo. Kwa maana naamini hayo yote ni wewe Mungu ndiye uyafanyaye, mara mbili, naam mara tatu, kwa mtu, ili kurudisha roho itoke shimoni [gizani], ili itiwe mwanga kwa mwanga wa walio hai [Ayubu 33:29-30], Amina.
No comments:
Post a Comment