#KUTENDA TENDO LISILOADILIFU NI DHAMBI NA KUTOKUTENDA LILILOADILIFU LILE LIKUPASALO KUTENDA NI DHAMBI PIA; HIVYO KATIKA YOTE KUWA MWADILIFU

Basi, mtu ambaye hafanyi lile jambo jema analojua kwamba anapaswa kulifanya, anatenda dhambi (Yakobo 4:17). Na pia kila tendo lisiloadilifu ni dhambi (1John 5:17) na ndio maana Biblia inasema katika 1 Yohana 3:4; Kila mtu atendaye dhambi anavunja sheria ya Mungu, maana dhambi ni uvunjaji wa sheria. Kule kutokuwa waadilifu, kutokuwa wachaji na watenda haki yaani kule kutokuwa waadilifu kwa wakati sahihi na mahali sahihi.

Jiweke karibu na Mungu (Yakobo 4:7-10)
Kwa hivyo; "Basi, jiwekeni chini ya Mungu; mpingeni Ibilisi naye atawakimbieni. Mkaribieni Mungu, naye atakuja karibu nanyi. Osheni mikono yenu enyi wakosefu! Safisheni mioyo yenu enyi wanafiki! Oneni huzuni, lieni na kuomboleza; kicheko chenu na kiwe kilio; na furaha yenu iwe huzuni kubwa. Nyenyekeeni mbele ya Bwana, naye atawainueni".

Eeh! Bwana mwingi wa neema na rehema [huruma na msamaha] nioshe mikono yangu na safisha moyo wangu kwa damu yako ya thamani ili niwe mchaji safi na huru hakika katika wewe; na hii ni sala yangu kuu ya kwamba Mungu niwezeshe na kuniongoza kwa uweza wa Roho Mtakatifu ili nitende mambo mema na sahihi kwa wakati sahihi na mahali sahihi, katika Jina la Yesu Kristo, Amina.

No comments:

Post a Comment