#MAISHA PASIPO ROHO WA MUNGU SI UZIMA HUO BALI KIFO

    Luka 22:35 naye Yesu wa Nazareti akasema,” nilipowatuma pasipo mfuko wa pesa wala mkoba wala viatu, mlipungukiwa na kitu chochote?” nao wanafunzi wake wakajibu,”La hasha! Hatukupungukiwa na kitu chochote,” Mistari wa 36; Yesu wa Nazareti akasema “lakini sasa, aliye na mfuko wa pesa auchukue na aliye na mkoba vivyo hivyo. Naye asiye na upanga,auze joho lake anunue mmoja.

Vivyo hivyo na wana wa Israeli chini ya uongozi wa Musa kwa miaka 40 walizunguka jangwani pasipo kupungukiwa na chakula kilichotoka mbinguni (mana) wala maji kwa ajili ya kupoza kiu zao, Nehemia 9:20-21 inasema”Ukawapa na roho yako mwema ili kuwaelimisha, wala hukuwanyima mana vinywani mwao, tena ukawapa maji kwa ajili ya kiu yao. Naam, muda wa miaka 40 uliwaruzuku jangwani, wasihitaji kitu; nguo zao hazikuchakaa, wala miguu yao haikuvimba,
Na pia katika kumbukumbu la torati 8:4 biblia inasema;”Mavazi yako hayakuchanika, wala mguu wako haukuvimba, miaka hiyo arobaini.” na 29:5 inasema;”Nami miaka 40 nimewaongoza jangwani; nguo hazikuchakaa juu yenu, wala kiatu chako hakikuchakaa katika mguu wako.

Kama ilivyokuwa kwa mpakwa mafuta wa Bwana, Musa wana wa Israeli waliruzukiwa na Mungu kwa miaka 40 jangwani pasipo kupungukiwa na kitu, ndivyo ilivyokuwa kwa mitume 12 wa Yesu wa Nazareti (kristo) waliambatana naye na kisha kufanana na Yesu wa Nazareti na kuwa kama yeye pasipokupungukiwa na kitu chochote biblia inasema hadi kuzungumza, kuvaa, kutembea, vyote vilifanana na Yesu wa Nazareti kwa miaka yote mitatu ya huduma ya Yesu wa Nazareti (kristo) duniani. Imani yao ilikuwa kubwa hata walipoambiwa wakachukue mwana punda hawakusita waliamini inawezekana na wakampata sawa sawa na walivyoagizwa na pia walipotumwa na Bwana waende mjini watakutana na mtu mmoja wamwambia Bwana atakuja kufanyia karamu chumba cha juu yeye na wanafunzi wake hawakusita waliamini ikawa.

Hata Yohana mbatizaji akiwa amejaa Roho mtakatifu mbingu zilifunguka na akasikia sauti kutoka mbinguni ikimwambia kwamba Yesu wa Nazareti ndio mwana mpendwa wa Mungu na ndio mwokozi wa ulimwengu.

Lakini wakati ule roho mtakatifu alipowaacha imani ilipungua ndani mwao, wakaanza kuona ugumu na uhaba katika kila kitu kwenye maisha yao.

Yohana mbatizaji akatuma wanafunzi wake wamuulize Yesu wa Nazareti kama yeye ndiye mwokozi wa ulimwengu au asuburiwe mwingine.

Hata wanafunzi wa Yesu wa Nazareti baada ya roho wa Mungu kukaa kando nao; Petro alimkana Yesu, Yuda alimsaliti Yesu na wengine waliishi kwa hofu na woga mkuu, walipungukiwa katika kila kitu hadi Petro akaamua kurudi kuvua samaki kama awali ambapo hakufanikiwa pia, waliweka nyavu pasipo kupata samaki hata mmoja, Cha ajabu Yesu wa Nazareti alivyowatokea hali wao hawakumtambua (baada ya kufufuka kwake) na kuwahakikishia kupata samaki wakuweka nyavu upande wa kulia wa mashua walipotii ndipo samaki walijaa hadi nyavu kutaka kukatika (Yohana 21:5-6) nao wakagundua ni Yesu wa Nazareti tu aliyeleta muujiza huo na ni kweli Yesu wa Nazareti ndiye aliyefanya, wakaufurahia uwepo wake uliojaa Baraka.

Hii pia inathibitika katika Biblia –Joshua 5:12 inasema;”Ndipo ile mana ikakoma siku ya pili yake baada ya wao kuyala hayo mazao ya nchi na hao wana wa Israeli hawakuwa na mana wala haikuonekana kwao tena, wakala katika vilima vya nchi ya kanani (kwa jasho lao) mwaka huo”

Kwa hivyo ndugu uzima wa kweli ni roho mtakatifu akiwa ndani yako. Neno hili linatupa upeo kuwa vitu vingi hubadilika roho mtakatifu akikaa kando nawe au akikuacha utaona maisha kuwa magumu, mambo yanakuwa hayaendi kama ulivyokusudia hamna kibali katika ya wanadamu wenzako, lakini hali inakuwa ni mbaya zaidi na ya kuchanganya katika yote uyatendayo ukigeuka nyuma na kuyarudia matapishi na kuiacha njia ya haki na kweli ambapo ndiko uliko uzima na mafanikio yote.

Simama imara katika Imani iliyothibitika kwako, Mwamini Yesu wa Nazareti maisha yako yote ni mwaminifu na wala hata kuacha uaibike, Amina.

No comments:

Post a Comment