#UKIRI WA MTU AMTEGEMEAYE YESU WA NAZARETI (BWANA NA MWOKOZI WETU)

    Mwanadamu aliyeumbwa na Mungu, ambaye amtumainia yeye na kumtegemea Bwana wetu Yesu Kristo wa Nazareti siku zote husema na kukiri Zaburi ya 23 kama ndiyo utambuzi na msingi wake kwamba Mungu kwake ni kila kitu katika maisha yake;

BWANA ndiye mchungaji wangu – HUO NI UHUSIANO NA MUNGU!
Sitapungukiwa na kitu – KWA MAANA YEYE NI MTOAJI!
Katika malisho ya majani mabichi hunilaza – HILO NI PUMZIKO!
Kando ya maji ya utulivu huniongoza – HICHO NI KIBURUDISHO NA AMANI YA ROHO!
Hunihuisha nafsi yangu – HUO NI UPONYAJI!
Na kuniongoza katika njia za haki - HUO NI MWONGOZO!
kwa ajili ya jina lake – HILO NI KUSUDI!
Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti – HILO NI JARIBIO!
Sitaogopa Mabaya – HUO NI UHAKIKA WA ULINZI!
Kwa maana Wewe upo pamoja nami – HUO NI UAMINIFU!
Gongo lako na fimbo yako vyanifariji – HIYO NI NIDHAMU YA MAMLAKA!
Waanda meza mbele yangu machoni pa watesi wangu – HAYO NI MATUMAINI!
Umenipaka mafuta kichwani pangu – HICHO NI KIBALI!
na kikombe changu kinafurika – HUKO NI KUTOPUNGUKIWA NA KITU!
Hakika wema na fadhili zitanifuata siku zote za maisha yangu – HIZO NI BARAKA!
Nami nitakaa nyumbani mwa BWANA – HUO NI UZIO!
Milele – HAPO NI MPAKA MWISHO!

Kwa maana hata katika Biblia (Zaburi 125:1) inazungumzia kuwa wamtumainio na kumtegemea Bwana (Yesu wa Nazareti) ni kama mlima sayuni hautatikisika milele daima, Amina.

No comments:

Post a Comment