#NGUVU YA KUMBUKUMBU

Hebu fikiria biblia inakitabu pekee cha kumbukumbu kwa ajili ya kukumbuka tu, ipo nguvu ndani ya kumbukumbu.

Kumb. 15:15; Siku zote kumbuka ulikotoka.

Saa nyingine kumbukumbu ni kama funguo au secret code au password ya kukuvusha ulipokwama, hata Eliya nabii alipotwaliwa Elisha Kwa kukumbuka alivyofanya Kwa imani akavuka Jordani.

Kumbukumbu za nyuma ndizo zitakazosaidia kunyoosha maisha yako ya baadae. Pale alipokutoa BWANA ni alama (mark) tosha ya kukurejeza upya kwa toba kila wakati siku zote.

Zaburi 137:1; Kumbukumbu 4:9; 8:12-18.

Naam! Ukikumbuka tu na kutubu, utarudi kwenye upendo wako wa kwanza na matendo ya kwanza (ufunuo 2:4-5).
Mch. Tetemeko Elisha -UMINA

No comments:

Post a Comment